Audio & Video

Naibu Waziri Mavunde atoa kauli ya serikali kuhusu ajira kwa watoto

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Serikali imewata wanajamii wakiwemo wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwatumikisha watoto katika ajira mbalimbali ili kujipatia kipato kwani hatua hiyo ni kinyume na sheria zinazomlinda mtoto.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Antony Mavunde alitoa kauli hiyo jana akiwa Jijini Mwanza kwenye maadhimisho ya siku ya kupinga ajira kwa watoto duniani yaliyondaliwa na shirika la kutetea haki za watoto wafanyakazi wa nyumbani WoteSwa.

Mkurugenzi wa shirika la WoteSawa, Angel Benedicto alisema bado watoto wanatumikishwa ambapo shirika hilo limebaini zaidi ya watoto elfu moja walioajiriwa kazi za nyumbani Jijini Mwanza huku akiomba serikali kufanya marekebisho katika sheria kadhaa kandamizi kwa watoto.

Mkurugenzi wa shirika la WoteSawa, Angel Benedicto akizungumza kwenye maadhimisho hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa JB Fairmont Hotel Jijini Mwanza. Maadhimisho hayo yalikwenda pamoja na uzinduzi rasmi wa tovuti ya Shirika la WoteSawa

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Mhe.Antony Mavunde (kushoto) akifuatilia kwa makini mada kwenye maadhimisho hayo. Kulia ni Mkurugenzi wa shirika la WoteSawa, Angel Benedicto

Wafanyakazi wa shirika la WoteSawa na mkuu wa wilaya Nyamagana wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi

Mpe Elimu Siyo Ajira

Tazama BMG Online TV hapa chini

SOMA Wafanyakazi wa nyumbani wafunguka kwa hisia

Recommended for you