Habari Picha

Manispaa ya Ilemela yapanda miti kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani

on

Judith Ferdinand, BMG

Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza imefanikiwa kupanda zaidi ya miti 17,000 katika kipindi cha mwaka 2017/2018, lengo likiwa ni kuhifadhi, kutunza na kuboresha mazingira.

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, John Wanga aliyasema hayo jana kwenye kilele cha Wiki ya Mazingira Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Juni 05 ambapo kiwilaya katika Kata ya Kawekamo.

Katika maadhimisho hayo, Wanga ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza pia aliongoza zoezi la upandaji miti na kubainisha kwamba halmashauri imepanda miche katika barabara ya Airport.

Aliwahimiza wananchi kuwa na utamaduni wa kutunza mazingira na kujiepusha na tabia ya ukataji miti ovyo ili kuendana na kauli mbiu ya mwaka huu isemayo “Mkaa ni gharama tumia nishati mbadala”  .

Afisa Mazingira Manispaa ya Ilemela, Simon Nzagi alisema maadhimisho hayo yameendana sanjari na upandaji miti  ya miembe ambayo itasaidia kupata kivuli na matunda ambapo walipanda miche 100 ambapo lengo ni kupanda miche 340.

Baadhi ya wananchi akiwemo Agness Lucas ambaye ni mkazi wa Kata ya Kawekamo waliomba kupatiwa elimu zaidi kuhusu matumizi ya nishati mbadala ili kuondokana na matumizi ya mkaa.

Mkurugenzi Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza akizungumza jana kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mazingira.

Mkurugenzi Wanga akizungumza kwenye maadhimisho hayo.

Manispaa ya Ilemela imepanda zaidi ya miche elfu kumi kwa kipindi cha mwaka 2017/18.

Mkurugenzi Wanga akishiriki zoezi la upandaji miti. SOMA Wafanyakazi wa TBL Mwanza wafanya usafi mto Mirongo

Recommended for you