Audio & Video

Miezi ambayo kuna hatari ya upungufu wa damu kutokea

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Juni 14 kila mwaka huwa ni Maadhimisho ya Siku ya Mchangia Damu Duniani ambapo mwaka huu ofisi ya Mganga Mkuu Mkoa Mwanza imeshirikiana na Ofisi ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama nchini kuadhimisha kilele cha maadhimisho hayo katika viunga vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanza Sekou Toure.

Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya Nyamagana Mhe.Marry Tesha aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza ambapo wananchi walihimizwa kuendelea kuchangia damu ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa damu hususani mwezi wa sita na wa 12 baada ya taasisi za elimu kuwa katika likizo kwani taasisi hizo zimekuwa na mwitikio mkubwa katika uchangiaji damu.

Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Mhe.Marry Tesha akifanya vipimo vya awali kabla ya zoezi la utoaji damu

SOMA Wenye sifa za kuchangia damu

Recommended for you