Audio & Video

Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika mkoani Mwanza

on

Judith Ferdinand, Mwanza

Tanzania hii leo imeaungana na nchi mbalimbali kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika ambapo kwa mkoa wa Mwanza maadhimisho hayo yanafanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari Sangabuye iliyopo Kata ya Bugongwa Manispaa ya Ilemela mkoani hapa.

Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya maadhimisho hayo ambaye pia ni Meneja Mradi wa Shirika la Railway Children Afrika, Abdalah Issa amesema maadhimisho hayo huadhimishwa kila mwaka Juni 16 ili kuwakumbuka watoto waliouwawa nchini Afrika Kusini wakidai haki zao.

Issa amesema kwa mwaka huu siku hii inaadhimishwa nje kidogo ya Jiji la Mwanza ili kuhamasisha na kuonyesha jamii umuhimu wa mtoto na kwamba anahitaji kupatiwa haki za msingi ikiwemo elimu.

Amesema kupitia maadhimisho hayo, jamii  hiyo itajengewa uwezo na uelewa wa kutambua umuhimu wa kuwapeleka watoto shule na kuacha kuwatumikisha kwenye shughuli mbalimbali ikiwemo uvuvi amba ndoa na hatimaye mimba za utotoni.

Kaulimbiu ya mwaka huu ni “Kuelekea uchumi wa viwanda, tusimwache mtoto nyuma”.

Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya maadhimisho hayo ambaye pia ni Meneja Mradi wa Shirika la Railway Children Afrika, Abdalah Issa. SOMA Siku ya Mtoto wa Afrika 2017

SOMA Siku ya Mtoto wa Afrika 2016

Recommended for you