Audio & Video

Wadau Jijini Mwanza wakumbushwa tena kuhusu watoto waishio Mtaani

on

Judith Ferdinand, BMG Habari

Jamii mkoani Mwanza kwa kushirikiana na serikali pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo, imetakiwa kushirikiana pamoja ili kuwalea watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi (mitaani).

Rai hiyo ilitolewa juzi na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi Jijini Mwanza katika  Maadhimisho ya Siku ya Watoto Wanaoishi na Kufanya Kazi Mtaani Duniani yanayoadhimishwa kila mwaka aprili 12.

Kwa mkoa wa Mwanza, maadhimisho hayo yalifanyika katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza kupitia uratibu wa Shirika la Railway Children Afrika wakishirikiana na Cheka Sana Tanzania na Upendo Daima.

Mtoto Jumanne Mussa alisema hatua hiyo itasaidia kuwezesha upatikanaji wa haki zao ikiwemo kulindwa na kusikilizwa kwani yapo madhara makubwa ikiwa watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani watatengwa na jamii.

Naye Khadija Majuto alisema changamoto wanazokutana wakiwa mtaani ni ukosefu wa chakula, kupingwa, kubaguliwa na kuitwa majina mabaya kama chokoraa, kukosa haki ya kupendwa, malezi na ulinzi pamoja na kunyanyaswa kingono na kijinsia.

Kaimu Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Mwanza, Edith Mokiwa alisema wazazi, walezi na polisi wanapaswa kushirikiana ili kuhakikisha wanazuia ongezeko la watoto kukimbilia mitaani kwa kila mmoja kutimiza ipasavyo wajibu wake.

Kwa upande wake Afisa Mradi kutoka shirika la Railway Children Africa, Eva Mushi alisema elimu inapaswa kuendelea kutolewa kwa jamii ili kuwa na mtazamo chanya kuhusu watoto wanaoishi mitaani na kwamba wazazi wanatakiwa kuwajibika ipasavyo katika malezi kwani watoto wanaenda mtaani kufuata mahitaji baada ya kuyakosa nyumbani

Hata hivyo Mrakibu Msaidizi wa Polisi Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Mwanza Betimasimbo Shija alisema wazazi wanapaswa kuchukua jukumu la kuwalea watoto na wakishindwa waende ustawi wa jamii kupata ushauri zaidi.

Soma zaidi HAPA ama tazama video hapo chini. 

Recommended for you