Habari Picha

SOMA MIPANGO NA MAANDALIZI YA NDOA YA MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI JOSHUA NASSARI INAYOFANYIKA LEO.

on

Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Mh Joshua Nassari anafunga ndoa na Bi Anande Nko katika kanisa la Pentekoste, Kilinga
lililoko wilaya ya Meru ambako Mh Nassari alianzia masuala ya Kiimani
ikifuatiwa na Sherehe kubwa ya Harusi itakayo fanyika katika viwanja vya
Usa-River Academy jirani na Hotel ya Ngurdoto.

 

Kwa
Mujibu wa Mh Nassari ,sherehe hizo zitakazoanza majira ya saa saba
mchana  watu wote wamealikwa wakiwemo ndugu, marafiki, Jamaa na wananchi
jimbo la Arumeru Mashariki kwenye tukio hilo na kwamba hakuna kadi.

“Nichukue
tena fursa hii kuwakaribisha ndg, marafiki, Jamaa na zaidi sana
wananchi wangu wa jimbo la Arumeru Mashariki kwenye tendo hadhimu la
kusherekea harusi yangu , Jumamosi Juni 7, Usa-River academy grounds
kuanzia saa saba mchana. Kwa Pamoja Tulianza na Mungu, Tutamaliza na
Mungu Pamoja. …No cards on entrance!” alisema Nassari.

Nasari
amesema watu zaidi ya 8000 wanatazamiwa kushiriki katika sherehe hiyo
ya aina yake wakiwemo viongozi mbalimbali na wabunge kutoka maeneo
mbalimbali .

Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua
Nassari akimwimbia mchumba wake Bi Anande Nnko wakati wa sherehe ya
Send off iliyofanyika nyumbani kwao na Bi Harusi Mtarajiwa
,Meru.