Habari Picha

SOMA UCHAMBUZI MAALUMU KUHUSU SERA YA MAENDELEO YA VIJANA NCHINI TANZANIA.

on

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Edwin Soko ambae ni Mchambuzi na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uharifu. Pia ni Mratibu wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Mwanza. (Picha Kutoka Maktaba-BMG)

1:Nini  Maana 
ya Sera?
Ni 
mpango, hunaoweza  kuandaliwa  na serikali, chama cha  siasa au biashara ikiwa inalenga  kutoa ushawishi utakaopelekea kufanywa  kwa 
maamuzi , vitendo na hatimaye 
kupata  mafanikio.
Sera  
ta  Taifa  ta 
Maendeleo  ya  Vijana 
inatoa  mwongozo  si  tu
kwa  vijana, wazazi  na waelimishaji bali  kwa 
jamii  nzima  na hasa 
kwa  wapangaji  wa mipango 
ya   maendeleo   katika 
sekta  mbalimbali za maendeleo.
2:Maana  ya kijana
Inaweza  kutofautiana 
kutokana  na mila, desturi na
tofauti za maadili  katika jamii  mbalimbali 
na mahali walipo. Kijana ni 
mvulana  au mwanamke  ambaye 
yupo  katika  rika la utoto 
kuelekea  rika la utu uzima.  Kuligana na 
tofauti  mbalimbali   sera 
hii  imetumia  fafsiri 
ya  kijana  kutokana na tamko la  Umoja wa Mataifa ambapo kijana  ni mtu 
mwenye  umri kati  ya 
miaka  14- 24.
3:Historia  hadi 
kutungwa kwa Sera
Tangu 
Tanzania  ipate  uhuru 
wake  mnamo   mwaka 1961 
hapakuwa na  Sera  rasmi  iliyoandaliwa  
kwa  ajili    ya 
malezi  na maendeleo  ya 
Vijana . Masuala  ya  malezi na maendeleo  ya 
vijana  kwa kipindi  chote hicho 
yalikuwa  yakitekelezwa  kupitia 
Sera  nyingine katika mipango  ya 
maendeleo, kampeni, maazimio  na
miongozo ya  chama tawala  na 
Serikali.
Sera hii iliandaliwa kwa ajili ya kusimamia maslahi ya kijana, ambayo serikali iliandaa mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007,  Sera ya taifa ya maendeleo ya vijana ya 2007 inalenga masuala ya maendeleo ya vijana ambayo ni pamoja na: uwezeshaji wa kiuchumi, mazingira, VVU na Ukimwi, jinsia, sanaa na utamaduni, michezo afya ya uzazi kwa vijana na masuala ya maisha ya familia.
4:Msingi
wa Sera
Msingi wa  sera  unatokana na uzingatiaji wa haki za binadamu
kama zilivyotajwa  katika  katiba 
ya  Jamhuri  ya 
Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 
na kufanyiwa  marekebisho  mwaka 1984 na 1995.  Haki 
hizi ni  pamoja  na haki 
ya  kuishi, kulindwa,
kuendelezwa  na kujiendeleza,
kushirikishwa  katika  shughuli za maendeleo  yake 
na  jamii. Haki  nyingine 
kulingana  na  katiba hiyo ni pamoja  na 
haki  ya kutobadiliwa ,
kuheshimiwa, kumiliki mali na rasilimali, kufanya  kazi 
na  kupokea  matunda 
ya  kazi  hiyo pamoja na mbele  ya sheria 
za Nchi.
4:Lengo  la 
Sera
 • Kuhakikisha Taifa linakuwa na
  vijana wenye uwezo, wenye ari ya kutosha , wawajibikaji na wanaoshiriki
  kikamilifu katika Nyanja zote za kijamii, kisiasa na kiuchumi kwa
  maendeleo ya jamii.
 • Kuweka mazingira yanayowezesha
  kujenga uwezo wa vijana na kukuza nafasi za ajira na kupata huduma ya
  hifadhi ya jamii
5:Uchambuzi
Sera  ina  sehemu   
kuu  Tano (5)
5:1 Sehemu ya kwanza:
Hii  inaeleza 
utangulizi    kwa mujibu wa  miongozo 
ya  kisera
5:2 Sehemu ya pili:
·        
Umuhimu wa sera
·        
Dhamira
·        
Dhima
·        
Malengo
5:3 Sehemu  ya  Tatu
Sehemu hii  imebeba  mambo (29) 
yakiwemo:
 • Mambo  kisera  na maelezo  yake
 • Tafsiri sahihi ya  
  kijana
 • Mzingira  ya  vija 
  kuishi  kwenye  dimbwi la matatizo
 • Maandalizi  ya  kijana 
  ili aishi kwa kufuata 
  misingi  ya  jamii
 • Rasilimali  zinazoweza
  kumwinua kijana  na  kumwendeleza
 • Huduma  za kifedha  zninazoweza kuondoa  umaskini kwa kijana
 • Ushiriki wa vijana 
  kwenye  kilimo  na 
  ufugaji
 • Nafasi za vijana 
  kwenye  serikali za
  mitaa   na uongozi wa Mkoa
 • Haki za kijana
 • Misingi ya usawa wa 
  kijinsia kwenye  maendeleo
 • Mifumo  ya
  kisheria  ya  kumwendeleza kijana
 • Vijana na sekta 
  ambazo  si  rasmi
 • Chombo  cha  kisheria 
  cha kuwaunganisha  vijana
 • Ushiriki wa kijana 
  kwenye  kumwelndeleza  kijana
 • Kijana  na  fursa 
  za  ajira
 • Vijana na madhira 
  ya  Ukimwi
 • Matumizi ya 
  TEHAMA  Kwa  vijana
 • Kijana  na ulemavu
5:4 Sehemu
ya Nne
-Majukumu  ya wadau
 • Wazazi na  walezi
 • Mashirika ya dini, taasisi
  zisizo  za kiserikali, sekta  binafasi 
  na asasi za kijamii
 • Serikali za Mitaa  na 
  uongozi wa Mkoa
 • Serikali kuu
 • Wadau wa maenedeleo
5:5 Sehemu
ya  Tano:
-Mpangilio wa utekelezaji
-Hupatikanaji wa huduma za kijamii
-Usimamizi wa 
program, ufutiliaji  na  tathimin
6:0 Mtazamo
Kimsingi  Suala 
la   Taifa  kuwa 
na  sera  ya 
Vijana   limechelewa  kwa 
kiasi  kikubwa  kwani tumepata  sera 
hiyo    mwaka 2007 
wakati wenzetu  Kenya  ilikuwa 
na sera  hiyo  mwaka ……………. 
Uganda  mwaka ……………..
Mwanasisasa  Zitto 
Kabwe  hakukosea  kusema 
kuwa  Taifa  hili ni 
Taifa  la  Vijana na watoto, kwani  kwa mujibu 
wa  sensa  ya 
watu  na  makazi   
Vijana  wamebeba  asilimia 
33/%   ya  watu 
wote.
Vijana  na 
Uchumi wa Nchi
Nchini   Tanzania 
vijana    wengi  wamekuwa 
wakijihusisha  katika  sekta 
za kilimo, uvuvi, madini, ufugaji 
na uwekezaji  kwenye  viwanda 
vidogovidogo  kama    utengenezaji wa  matunda, vitua 
asilia na  vinginevyo.
UCHAMBUZI
Kwa
kiasi  kikubwa  sera  
imeakisi  matatizo  ya 
vijana   wa kitanzania  na 
pia  kutoa  mwelekeo 
mzuri  sana  wa kuyashughulia  matatizo 
hayo.
Mfano:
Suala  la 
ajira  kwa  vijana
Kama  tujuavyo 
kuna  vijana  wengi 
wanaomaliza  elimu  ya msingi, sekondari  na 
vyuo  vya  juu 
wakikosa  ajira   na kuangukia kwenye  sekta 
zisizo  rasmi, ambazo  huko 
hakuna   job  security, kukosekana kwa mitaji  
Kauli  ya 
sera
 • Serikali  kwa 
  kushirikiana  na  sekta 
  binafsi  itaandaa  mazingira  mazuri 
  ya  kutengeneza  ajira 
  kwa  vijana.
 • Kuwa  na sera 
  ya  Taifa  ya 
  ajira
 • Kuwa  na sera 
  ya  undelezaji  maeneno 
  ya vijijini na kilimo (Rural Development Strategy and
  Agricultural Development Policy.
 • Serikali  kushirikiana  na 
  taasisi  binafsi   na wadau  wengine 
  kutoa  elimu ya  ujasiriamali  kwa 
  vijana  ili waweze kujiajiri.
Ushirikishwaji
wa  vijana  na 
Utawala  Bora
Vijana    wanamchango 
wa 65%    ya  nguvu kazi 
ya  wazalishaji wa  uchumi wa 
Taifa (Labour  Force)  lakini   
35%    ya  vijana 
hao  hawawakilishwi  vyema kwenye 
forums  mbalimbali za ngazi  ya 
maamuzi, na matokeo  yake  maamuzi 
mengi yanayofikiwa  hayagusi  matatizo 
ya  vijana.
Kauli  ya sera
Mifumo   ya 
halamashauri za    serikali za
mitaa  na 
serikali  kuu  iwe  na
mifumo  inayotambua  uwepo wa jina 
na  pia  uwakilishi 
kwenye  ngazi  nyingine 
za kitaifa  na kimataifa
Kuwa  na 
chombo cha  kuwaunganisha  vijana
Kwa
muda  mrefu  kulikuwa   
hakuna  chombo  chenye 
nguvu  kinachoweza kuwaleta  vijana 
pamoja na kutambua  matatizo   yao.
Kauli  ya 
sera 
Kuundwa  kwa 
chombo kitakachoweza kuwasemea 
vijana “ Uuundwaji  wa  Baraza 
la Vijana Taifa”
Huduma  za kifedha 
na mkakati wa  kupunguza  umaskini
Kuna  mikakati mingi  iliyopitishwa 
kwenye  kuwainua  vijana kwa kuwapa misaada   ya  kifedha
ili waweze  kujiinua  kiuchumi, lakini  mikakati hiyo 
imekuwa  si  endelevu, wala  mpangilio 
mzuri
Kauli
ya    sera
 • Kuwa  na mkakati  endelevu 
  wa  kuwasaidia  vijana kifedha  ili waweze kujiinua  kiuchumi
 • Kusisitiza  umuhimu wa kuwa na mfuko wa  wa 
  fedha  wa kuwasaidia  vijana.
Nafasi  ya 
vijana  kwenye  muundo wa 
Serikali za mitaa
Muundo
wa  Serikali  za mitaa  
hakuweza  kuwa  na uwakilishi 
mzuri  wa  kutambuamatatizo  ya vijana, kwa kuwa  hakukuwa 
na Afisa    anayeshughulikia   uendelezi 
wa kada  ya   vijana, hii 
ilifanya  kuwa  na mfumo 
dhaifu  toka  serikali 
kuu  hadi  serikali 
za mitaa.
Kauli
ya  Sera:
 • Kuwe  na up – 
  down   approach   wa kutoa  uwakilishi  toka  
  ngazi za  kata  hadi 
  Taifa, hilo  liwe  jukumu 
  la  wizara    husika 
  ya serikali za mitaa na 
  serikali  kuu
 • Serikali  kuu 
  na serikali za mitaa iweke 
  utaratibu  wa kuajiri  Afisa 
  atakayehusika  na undelezaji
  wa kada  ya  vijana
Vijana  kuishi 
kwenye  mazingira  magumu
Kuna  vijana 
wapatao  million  2 
yatima  wanaoishi kwenye  mazingira 
magumu sana  ya kimaisha
Kauli  ya sera
Sera  imeelekeza kuwa, kuna  mkakati 
wa kuwawezesha  kupata  fursa 
kwenye  elimu, mafunzo na
usalama  wao kwa wote  waliokubwa na 
matatizo  hayo.
Maandalizi  kwa kijana 
ili  awe  raia 
mwema  kwenye  jamii
Vijana  wametakiwa 
kuwa   na  maandalizi 
mazuri  ili waweze  kutimiza 
wajibu wao  kwenye  jamii wa kuwa 
raia  wema.
Kauli
ya  sera
Kuwa  na 
mkakati  maalumu  wa kuandaa 
miongozo  ya  malezi 
kwa  vijana
Matumizi  ya 
rasimimali za Nchi  zinazoweza
kuwainua  vijana
Tunaelewa  wote 
kuwa  Nchi  yetu ina rasilimali nyingi, ambazo  zikitumika 
vizuri  zinaweza  kuwasaidia sana  vijana 
kuinua  maisha  yao. 
Rasilimali  hizo  ni 
kama  ardhi na nyinginezo
Kauli  ya 
sera .   Kwa mujibu wa      integrated   labour  
survey 2001,  asilimia  65 
ya  wazalishaji  wa 
uchumi  wa Nchi ni  Vijana.
Kauli  ya 
sera
Kutakuwa  na 
kipaumbele  cha  rasimimali za 
Nchi  kwa kundi la  vijana
Matumizi
ya    TEHAMA
Vijana
wengi  wamekuwa  wakitumia 
teknolojia  kwa  mtazamo  
hasi  badala  ya 
chanya, kama kutumia  kwa  kukuza weledi wa kitaaluma    wao 
wanatumia kwa    kutazama  vitu 
vinavyoweza  kumomonyoa  maadili ya 
Taifa
Kauli
ya  sera
Kuwa  na 
makakati wa  kufuatilia  maudhui 
ya  matumizi  ya 
teknolojia
Mapungufu/Gap
Sera  yetu   
ina  mapungufu machache  kama 
kutoweka   kipaumbele  kwa makundi 
maalumu,  hii  inasababisha 
baadhi  ya  makundi 
Kutopewa kipaumbele,  Sera  ya 
maendeleo  ya  vijana 
ya  Kenya  yenyewe 
imeweka vipaumbele  kwa  makundi 
maalumu  ya vijana  kama walemavu, waathirika  wa HIV, wanawake, vijana  wasio na ajira  na 
wale waliokosa  fursa za kusoma.
HITIMISHO
Sera  ya 
Maendeleo  ya  vijana  ni 
nzuri  kwani  imeanisha 
matatizo  ya  vijana 
na kutoa  njia  sahihi 
ya  kuyashughulikia,  tatizo 
kubwa   linalojitokeza  hapa 
ni  kama  matatizo 
ya  sera  nyingine 
za Nchi hii suala  zima  la 
utekelezaji  wa sera
(Implementation) tu.
Endapo  Serikali 
ya  awamu  ya 
tano  itaamua  sasa 
kuisimamia  sera  hii 
kwa kuitekeleza  ni wazi  kuwa  
kijana    kada  ya 
vijana    itaboreka na kutoa  mchango 
mkubwa  kwenye     falasa 
ya  seriklai  ya 
John  Pombe   Magufuli  ya 
kwenda kwenye  uchumi wa  kati wa 
Viwanda.
Naomba  kuwakilisha
Edwin
Soko
PhD  Candidate  

Kumbuka Soko amewasilisha Uchambuzi huu hii leo katika Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza. TAZAMA HAPA.

Recommended for you