Audio & Video

Taasisi ya APHFTA yatoa mafunzo kwa Wataalam wa Maabara mkoani Geita

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Wataalam wa Maabara wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia weledi na taratibu za kiafya ili kuhakikisha wanatoa majibu sahihi ya vipimo na kusaidia utoaji wa dawa stahiki kwa wagonjwa badala ya kutanguliza maslahi binafsi.

Mwakilishi wa Mganga Mkuu mkoani Geita, Paul John ametoa rai hiyo leo wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalam wa maabara, zahanati na vituo vya afya kuhusu kipimo cha haraka cha kupima Malaria (MRDT), yaliyoandaliwa na Chama cha Watoa Huduma za Afya Binafsi Tanzania (APHFTA).

Mafunzo hayo yalianza jana na kutamatika leo Oktoba 02, 2018 ambapo wiki iliyopita pia APHFTA ilitoa mafunzo kuhusu mwongozo mpya wa kitaifa wa kudhibiti Malaria kwa madaktari na manesi mkoani Geita, hizo zikiwa ni juhudi za kupambana na ugonjwa huo.

Mwaka 2015/16 mkoa Geita ulikuwa na maambukizi asilimia 38 hivyo juhudi hizo zimesaidia kupunguza maambukizi hayo hadi kufikia asilimia 17.3 mwaka 2017/18

Mwakilishi wa Mganga Mkuu mkoani Geita, Paul John akifungua mafunzo hayo.
Mkufunzi kutoka Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria ambaye pia ni Mratibu wa Malaria mkoani Singida, Dkt. Abdallah Balla akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo.
Meneja Mradi wa kudhibiti Malaria mkoani Geita kutoka taasisi ya APHFTA, Bigeso Makenge akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Mratibu Malaria mkoani Geita, Gabriel Wangese ambaye pia alikuwa mkufunzi kwenye mafunzo hayo akifafanua jambo.
Mkufunzi Thomas Ngasa (kushoto) akitoa ufafanuzi namna ya kumuandaa mgonjwa kabla ya kumfanyia vipimo vya Malaria.

Recommended for you