Audio & Video

Taasisi ya APHFTA yatekeleza Vyema Mpango wa Kuzuia Magonjwa Yasiyoambukiza Mashuleni

on

Inaelezwa kwamba hadi kufikia mwaka 2020 magonjwa yasiyoambukiza yanaweza kusababisha asilimia 73 ya vifo kote duniani ikiwa hatua madhubuti hazitachukuliwa katika kupambana na magonjwa hayo ikiwemo Kisukari.

Ni kutokana na athari za magonjwa hayo, Chama cha Watoa Huduma za Afya Tanzania APHFTA, kikazimia kuanzisha Mpango wa Kitaifa wa Afya Mashuleni, lengo likiwa ni kupambana na magonjwa hayo ambapo mpango huo unafadhiriwa na Taasisi ya “World Diabetes Foundation” ya nchini Denmark.

Na ili kujionea utekelezaji wa mpango huo, jumatatu Novemba 20,2017 ulifanyika ukaguzi katika baadhi ya shule za msingi zinazonufaika na mpango huo Kanda ya Ziwa ambazo ni shule ya msingi Town na Bugoyi B za Mjini Shinyanga pamoja na shule ya msingi Isenga D iliyopo Ilemela Jijini Mwanza, na hakika wanafunzi wakaonekana kunufaika na mpango huo.

Meneja Miradi kutoka taasisi ya Word Diabetes, Bent Lautrup-Nielsen (kushoto), akizungumza kwenye ziara ya kujionea utekelezaji wa mpango huo mkoani Shinyanga.

Wanafunzi wa shule ya Msingi Town Mjini Shinyanga, wakiimba Ngonjela wakati wa ziara hiyo.

Viongozi mbalimbali kwenye ziara hiyo.

Wanafunzi wa shule ya Msingi Bugoyi B, Mjini Shinyanga wakiimba wakati wa ziara hiyo.

Meneja Miradi kutoka taasisi ya Word Diabetes, Bent Lautrup-Nielsen, akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Bugoyi B, Mjini Shinyanga.

Meneja Miradi kutoka taasisi ya Word Diabetes, Bent Lautrup-Nielsen (katikati), akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Bugoyi B.

Mratibu wa APHTA Kanda ya Ziwa, Dr.Joyce Mwihava akizungumza baada ya kuwasili shule ya msingi Isenga D, iliyopo Ilemela Jijini Mwanza, wakati wa ukaguzi wa mradi wa kuzuia magonjwa yasiyoambukiza mashuleni.

Meneja Miradi kutoka taasisi ya Word Diabetes, Bent Lautrup-Nielsen, akizungumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Isenga D Jijini Mwanza.

BMG Habari, Pamoja Daima!

Recommended for you