Habari Picha

Takukuru yatoa tahadhari kwa wagombea kwenye chaguzi za marudio

on

Judith Ferdinand, Mwanza

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Mwanza, imewataka wagombea kujiepusha na vitendo vya rushwa, hasa katika kipindi cha  uchaguzi mdogo  unaotarajiwa kufanyika Novemba 26 mwaka huu kwa baadhi ya kata nchini.

Hayo aliyasema jana Ofisa  wa TAKUKURU, Maua Ally   ambaye alimuwakilisha Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza, Ernest Makale katika ufunguzi wa  kampeni  ya uchaguzi  mdogo wa  madiwani katika uwanja wa Machinjioni, Kata ya Mhandu Jijini Mwanza.

Alisema  kipindi cha kampeni wagombe hutoa ahadi nyingi  ambazo hazitekelezeki kwa  wananchi  na hatimaye kuleta migogoro baada ya uchaguzi.

Hata hivyo alisema  ni vema  kila wananchi kutambua umuhimu wa kura zao kwa kujiepusha na vitendo vya kupokea  rushwa kwa wagombea   sambamba na  kuchagua viongozi wenye nia, sifa na uchungu wa kuleta maendeleo katika maeneo yao.

“Kifungu  cha sheria namba 23 kinakataza mtu yeyote  kugharamia  wapiga kura  usafiri wa aina yoyote katika kipindi cha  kampeni, kutoa zawadi , kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria,”alisema Ally.

Hata hivyo alisema, rushwa katika  kipindi cha kampeni na uchaguzi inaathiri mchakato  mzima wa demokrasi ya uwakilishi wa  maendeleo ya taifa  ikiwemo  kunyima  mpiga kura  haki ya  kumchagua mgombea anaye mtaka.

Naye Mgombea wa Udiwani wa kata ya Mhandu, kupitia Chadema Godfrey  Faustine
alisema, atahakikisha   ana  kukutana na wananchi ili kuweza kutatua   changamoto zinazowakabili.

Aidha alisema, kata hiyo   inakabiliwa na  changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa madawati na madarasa,  ili kuweza kupunguza msongamano wa wanafunzi, pia  atahakikisha  anaboresha michezo katika shule zilizopo katani hapo.

Kwa upande  wake  Katibu Bara za la vijana  Chadema (BAVICHA), Mkoa wa Mwanza  Boniphace Nkobe alisema,katika  kampeni  ni vema  kujenga hoja  ambazo zinamashiko  na kuacha na majungu ambayo hayana maana katika kusukuma gurudumu la maendeleo.

“Nawaomba wananchi wachague  kiongozi ambaye ataleta maendeleo katika maeneo yao,  kwani unapoenda kununua bidhaa sokoni  lazima  kungalia inayofaa  na kuuzika  hivyo basi mgombea  anasifa za kuitwa  diwani, pia naliomba jeshi la polisi kufanya kazi ya kulinda usalama katika kampeni na kuachana na   mambo ya siasa kwa sababu  hayawahusu,”alisema Nkobe.

Recommended for you