Audio & Video

Serikali kuboresha Kituo cha Makumbusho Bujora mkoani Mwanza

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Serikali imeahidi kufanya maboresho katika Kituo cha Makumbusho ya Utamaduni wa Wasukuma Bujora kilichopo Kisesa wilaya ya Magu mkoani Mwanza ili kukuza na kuendeleza utamaduni wa kabila hilo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe alitoa ahadi hiyo jana kwenye ufunguzi wa tamasha la jadi, mila na desturi za kabila la Wasukuma Bulabo ambalo hufanyika kila mwaka kusherekea sikukuu za mafuno likienda sambamba na ibada ya Karista Takatifu ya Kanisa Katoliki.

Awali akizungumza kwenye tamasha hilo lililoambatana na maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kituo cha Bujora, Mkurugenzi wa kituo hicho Padri Fabian Mhoja aliomba serikali kutoa ushirikiano zaidi ili kufanya maboresho ya miundombinu mbalimbali kituoni hapo.

Naye Katibu wa Watemi wa Kisukuma, Chifu Charles Itale aliipongeza serikali ya awamu ya kwanza kwa kusaidia kurejeshwa nchini fuvu la Mtemi Mkawa na kuiomba serikali ya awamu ya tano kusaidia kurejeshwa fuvu la Mtemi wa Bujashi lililopo Ujerumani.

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella alisema serikali itaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha inatunza kituo cha Bujora ambapo ni kituo pekee cha kurithi utamaduni wa kabila la Wasukuma nchini.

Ibada ya Karista Takatiku ya Kanisa Katoliki Bujora wilayani Magu.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akitoa salamu zake baada ya ibada ya Ekaristi Takatifu ya Kanisa Katoliki. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella na kulia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Makumbusho Bujora Padri Fabian Mhoja.

Waziri Mwakyembe akitembelea maeneo mbalimbali ya Kituo cha Makumbusho Bujora wilayani Magu.

Miongoni mwa maeneo ya kumbukumbu katika kituo cha Bujora.

Wananchi na waumini wa Kanisa Katoliki wakifuatilia ibada ya Ekaristi Takatifu.

Burudani za asili kutoka kabila la Wasukuma.

Tamasha la Bulabo litafikia kilele jumapili ijayo Juni 10, 2018 uwanja wa michezo Kisesa wilayani Magu.

Makundi hasimu ya ngoma za asili, Bagika na Bagalu huchuana vikali kwenye tamasha hili.

Watemi mbalimbali wa Kabila la Wasukuma wakifuatilia uzinduzi wa tamasha la Bulabo.

Watemi mbalimbali wa Kabila la Wasukuma wakifuatilia uzinduzi wa tamasha la Bulabo.

Mwenyekiti wa Machifu wa Kisukumba, Chifu Charles Kafipa (kushoto), akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella (kulia).

Wageni mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa UWT mkoani Mwanza, Hellen Bogoya (kushoto) ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti Kamati ya Maandalizi tamasha la Bulabo 2018.

Viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella wakicheza ngoma ya Kisukuma kwenye tamasha hilo.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula (katikati), pamoja na Mwenyekiti wa UWT mkoani Mwanza Hellen Bogoya (kulia) wakifurahia mchezo wa nyoka kwenye tamasha hilo.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula na mbunge wa Jimbo la Ilemela.

Mkurugenzi wa kituo hicho Padri Fabian Mhoja akizungumza kwenye tamasha hilo.

Katibu wa Watemi wa Kisukuma, Chifu Charles Itale (kulia) akisoma risala kwa niaba ya Watemi wa Kisukuma.

Katibu wa Watemi wa Kisukuma, Chifu Charles Itale (kushoto) akimtawaza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (kulia) kuwa Chifu wa Kisukuma ambapo alipewa jina la Manju Mkuu ambaye ni kiongozi wa ngoma kubwa ya Masanyiwa kwa kabila la Wasukuma.

Waziri Mwakyembe akipiga ngoma kuashiria uzinduzi wa tamasha la Bulabo mwaka 2018.

Tazama BMG Online TV hapa chini 

SOMA Salamu za RC Mwanza kwenye kilele cha Ufunuo wa Matumaini

Recommended for you