Audio & Video

MWANZA: Mshindi tamasha la Bulabo apatikana baada ya mtifuano mkali

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Tulia Ackson jana jumapili Juni 10, 2018 alihitimisha tamasha la ngoma za asili za kabila la Wasukuma Bulabo 2018 katika uwanja wa Kisesa Magu mkoani Mwanza.

Tamasha hilo lilianza jumapili iliyopita Juni 03, 2018 ambapo ngoma mbalimbali za asili zilichuana vikali huku ngoma ya Cecilia Bujora ikibuka mshindi wa kwanza na kujinyakulia zawadi ya ng’ombe mmoja na shilingi elfu hamsini, mshindi wa pili ngoma ya Buyeye Isesa iliyojishindia shilingi laki mbili na mshindi wa tatu ngoma ya Mchomoko iliyojishindia shilingi laki moja.

Mhe.Dkt.Ackson ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye tamasha hilo alitoa shilingi milioni mbili kwa ajili ya kukarabati kituo cha Bujora, shilingi milioni moja kwa ajili ya zawadi kwa machifu wa Usukuma na shilingi laki nne zawadi kwa vikundi vilivyoshiriki ngoma.

Aidha umoja wa Watemi wa Usukuma ulimtunuku Mhe.Dkt.Tulia Ackson cheo cha Mama wa mila na desturi zilizo njema na kumopa jina la Solanyiwa lenye maana ya Mteuliwa.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella alisema serikali itaweka mikakati ya kushirikiana na uongozi wa kituo cha Bujora ili kuboresha kituo hicho na kulinda utamaduni wa taifa.

Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Tulia Ackson akizungumza kwenye kilele cha ngoma za Bulabo 2018

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella akizungumza kwenye hitimisho la ngoma za Bulabo

Mkuu wa Wilaya Magu Mhe.Khadija Nyembo akizungumza kwenye kilele hicho cha tamasha la Bulabo 2018

Mhe.Shibuda akitoa salamu zake kwenye tamasha hilo

Kulia ni Katibu wa Umoja wa Watemi wa Usukumaji, Chifu Charles Itale akisoma taarifa ya umoja huo kabla ya kumtunuku Naibu Spika jina la Solanyiwa. Kushoto ni Mtemi Nyamilonda wa tatu.

Umoja wa Watemi wa Usukumani umemtunuku Mhe.Dkt.Tulia Ackson cheo cha Mama wa mila na desturi zilizo njema na kumpa jina la Solanyiwa lenye maana ya Mteuliwa

Huyu aliingia na paka akiwa hai

Cecilia Bujora waliingia na nyoka

Watoto wa shule ya msingi Bujora nao walipewa nafasi ya kuonyesha ujuzi

Wapenzi wa ngoma za asili kutoka ndani na nje ya nchi walijitokeza

Zawadi

Naibu Spika Mhe.Dkt.Tulia Ackson (kulia), akiteta jambo na Mwenyekiti wa Machifu wa Usukuma, Chifu Charles Kafika (kushoto). Katikati ni Mwenyekiti wa UWT mkoani Mwanza Hellen Bogohe ambaye pia alikuwa Makamu Mwenyekiti Kamati ya Maandalizi tamasha la Bulabo 2018

SOMA Ufunguzi Tamasha la Bulabo 2018

Recommended for you