Burudani

Tamasha la “Lakwetu Concert” kutikisa Jijini Mwanza 2017

on

Judith Ferdinand, Mwanza

Lakwetu Concert kutikisa mkoani  Mwanza, siku  tatu mfululizo, msimu huu wa kusherekea siku kuu ya  Christmas, kwa  wakazi wake kupata burundani kutoka kwa waimbaji mbalimbali  wa mziki wa injili.

Tamasha hilo limeandaliwa na  Famara Promotions & Entertainment, ambalo ni  msimu wake wa pili, litafanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba ambapo wambaji mbalimbali wa nyimbo za injili watatumbuiza  na kuwaburudisha  wakazi wa jiji la Mwanza.

Akizungumza na BMG, Mratibu wa tamasha hilo Fabian Fanuel alisema tamasha litafanyika kwa siku tatu Disemba 24 hadi 26 kuanzia saa saba mchana mpaka 12 jioni ambapo takribani waimbaji 200 watatumbuiza ambapo 150 wataimba sikukuu ya Christmas na 50 siku ya kufungua Zawadi (boxing day).

Fanuel alisema Jumapili Disemba 24  itakuwa LAKWETU Talent Star Search na semina kwa wasanii wote, jumatatu Disemba 25 itakuwa LAKWETU Concert Christmas Fever huku  Jumanne Disemba 26 itakuwa LAKWETU Concert Boxing Fever.

Pia alisema mgeni rasmi siku ya Christmas atakuwa Flora Lauwo ambaye ni Mkurugenzi wa Nitetee Foundation, Flora Show na Salon huku siku ya boxing day atakuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza James Bwire, ambao watasindikizwa na wageni mbali mbali.

Aidha alisema wachungaji maaskofu  na waumini wa madhehebu mbalimbali wamekaribishwa, hivyo ni fursa ya wakazi wa jiji la Mwanza kupata burudani kupitia injili msimu huu wa sikukuu na kiingilio ni shilingi 1000.

Recommended for you