Audio & Video

Watapata raha sana kutumia Reli na Bandari za Tanzania

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP limeziamini njia za reli na bandari za Tanzania na kuamua kusafirishia makontena yake 18 ya chakula kwenda nchini Sudan Kusini kwa ajili ya wakimbizi ambapo msaada huo umetolewa na watu wa Marekani.

Treni iliyobeba makotena hayo ilifaulishwa Julai 03, 2018 katika bandari ya Mwanza ikitokea Jijini Dar es salaam na kuingizwa katika meli ya MV.Umoja ili kusafirishwa hadi bandari ya Portbell nchini Uganda tayari kuendelea nchini Sudani Kusini.

Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella walishuhudia tukio hilo muhimu ikiwa ni mara ya pili mzigo wa makotena kufaulishwa kupitia bandari ya Mwanza ambapo mara ya kwanza mzigo wa makontena ulifaulishwa Juni 24, 2018 baada ya miaka 10 tangu huduma hiyo isitishwe ambapo iliezwa kwamba watakaotumia reli na bandari za Tanzania watapata raha sana huku watakaojaribu kukwamisha juhudi hizo wakipata tabu sana.

PIA SOMA Uzinduzi wa huduma katika bandari ya Mwanza Kusini hadi Portbell Uganda

Recommended for you