Habari Picha

TAS wamuangukia Rais Magufuli

on

Na Ocsar Mihayo- BMG Habari

Chama cha Watu Wenye Ualibino Mkoa wa Mwanza (TAS) kimemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli kuhakikisha ana tia saini hukumu ya kunyongwa hadi kufa kwa watuhumiwa waliokutwa na hatia ya kuuwa na kuwatia ulemavu watu wenye ualibino.

Ombi hilo lilitolewa Jana na mwenyekiti wa Chama hicho Alfred Kapole wakati wa kikoa Cha kuwajengea uwezo Jamii juu ya kuishi na watu wenye ualibino katika Kijiji cha Kitongosima Wilaya Magu kilichoandaliwa na taasisi ya Disability Relief Service (DRS).

Kapole alisema kuendelea kuwepo magerezani kwa watu hao ndo maana vitendo hivyo haviishi na wao wanaendelea kuishi kwa hofu kubwa na matukio yanaongezeka kutokana na wahusika kutokuwa na hofu.

“Sisi tuna uchungu Sana maana wenzetu wanauwawa kwa ukatili mno ikiwa wauwaji wanajiandaa kabisa kutekeleza unyama huo hivyo kwa nini waendelee kutumia kodi yangu huko magerezani huku wakiwa wanaendelea kukutana na familia zoa huku wenzetu wamelala peke yao huko kaburini,” alilamika Kapole.

Kwa upande wake Viviani Kori Afisa mradi kutoka DRS alisema wataendelea kupambana ili kuhakikisha jamii inawatumbua na kuishi nao kama ndugu kwa kuunda Kamati zenye uwezo wake kujenga hoja kwenye midahalo, mikutano ya hadhara misikitini, makanisani na kwenye majukwaa ya wana siasa.

Kori pia alisisitiza kutembelea kambi za uvuvi na kuelimisha juu ya kuondoa dhana potofu kwamba viungo vya binadamu Hawa vina viashiria vya kuvuta samaki wengi wanapokuwa kwenye shughuli zao za uvuvi.

Naye mjumbe wa kikao hicho Peter Manyecha mwanafunzi wa kidato cha tano na mlemavu wa ngozi alilipongeza shirika hilo kwa kuendelea kupambania haki zao huku akiwa na ndoto za kuwa mwanasheria ili kuhakikisha ana pambana na watu wanaendelea kuwatia hofu na kuwafanya kuishi kwa mashaka.

Recommended for you