Audio & Video

Wajasiriamali mkoani Mwanza wapatiwa semina na TBS

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Shirika la viwango chini TBS leo Juni 11, 2018 limetoa semina kwa wajasiriamali zaidi ya 100 mkoani Mwanza, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kuzalisha bidhaa zenye bora.

Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora TBS, Nickonia Mwambene amesema kupitia semina hiyo, wajasiriamali wataweza kukidhi vigezo vya ubora na hivyo kupata fursa ya kimasoko ndani na nje ya nchi ikiwemo Kenya.

Baadhi ya washiriki wa semina hiyo iliyofanyika Jijini Mwanza wamesema yatawasaidia kuondokana na changamoto  zilizokuwa zikiwakabiri na kwamba wametakiwa umuhimu wa kusajili bidhaa na nembo za biashara zao.

Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora TBS, Nickonia Mwambene akizungumza kwenye semina hiyo

Kaimu Mkuu Ofisi ya TBS Kanda ya Ziwa, Joseph Makene akiwasilisha mada kwenye semina kwa wajasiriamali mkoani Mwanza

Afisa Viwango TBS, Stephanie Kaaya akiwasilisha mada kuhusu viwango vya bidhaa kwenye semina kwa wajasiriamali mkoani Mwanza

Afisa biashara mkoani Mwanza, Yessaya Sikindene akizungumza kwenye semina hiyo

Mmoja wa washiriki akichangia mada kwenye semina hiyo iliyofanyika ukumbi wa mikutano, ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.

SOMA WAJASIRIAMALI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA KUTOKA TBS

Recommended for you