Audio & Video

TEIC 2017 Get Together Party Dodoma

on

Mkutano wa wadau wa sekta ya uziduaji (Madini, Mafuta na Geisi) umetamatika Mjini Dodoma, huku baadhi ya maazio ya mkutano huo yakiwa ni asasi za kiraia kushiriki na kushirikishwa ipasavyo katika mijadala ya inayohusu manufaa ya rasilimali za taifa.

Baada ya mkutano huo wa siku mbili kuanzia Novemba 02,2017 kutamatika katika ukumbi wa St.Gasper, ilifuatia hafla ya jioni iliyofanyika Royal Village Hotel ambapo washiriki kutoka asasi mbalimbali ndani na nje ya nchi walijumuika pamoja.

Mkutano huo huandaliwa na umoja wa asasi zinazojihusisha na masuala ya utawala bora nchini uitwayo HakiRasilimali ambapo asasi hizo ni pamoja na ADLG, Governance Link, HakiMadini na Policy Forum.

BMG Habari, Pamoja Daima!

Recommended for you