Audio & Video

Timu ya Blue Eagles ya Jijini Mwanza yaanza kujinoa kwa kasi kubwa

on

Wachezaji wa timu ya Blue Eagles FC ya Jijini Mwanza wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Mwenyekiti wa timu hiyo, Alfred Mpemba.

Judith Ferdinand, BMG

Timu ya soka ya Blue Eagles ya Jjini Mwanza imeanza rasmi maandalizi ya mashindano ya Ligi Daraja la Nne yanayotarajia kutimua vumbi hivi karibuni katika uwanja mkongwe Nyamagana.

Akizungumza na BMG, Nahodha wa timu hiyo Edison Raymond amesema maandalizi yameanza vyema na lengo ni kuchuka ubingwa katika ligi hiyo.

Raymond anasema kutokana na maandalizi hayo, wachezaji wako vizuri na wanatarajia kuchukua ubingwa katika ligi na hivyo kuitangaza timu hiyo.

 “Katika mechi tulizokuwa tukicheza tumetambua kuna mapungufu mengi kwa wachezaji wetu na tunaendelea kuyafanyia kazi, nawaomba wadau wa soka Jijini wajitokeze kuipasapoti timu yetu kwani bila wao haitafanikiwa” Anasema Raymond.

Mwenyekiti wa timu hiyo, Alfred Mpemba anasema timu hiyo imeandaa wachezaji zaidi ya 25 ambao watashiriki katika ligi hiyo ili kuweza kufanya vizuri katika mashindano hayo.

Tazama HAPA Michuano ya Compassion 

Recommended for you