Michezo

Timu ya Habari Fm yaionea timu ya Chuo Kikuu Huria Mwanza

on

Wachezaji wa Open University wakisalimiana na wachezaji wa Habari FC kabla ya kuanza kwa mchezo wa kirafiki hapo jana katika uwanja wa Nyamagana.

Judith Ferdinand, Mwanza

Hayawi hayawi lhatimaye yamekua baada ya timu ya Habari FC kutoa kichapo cha goli 5-3, dhidi ya Chuo Huria (Open University), cha jijini Mwanza.

Katika mchezo  wa  kirafiki ambao ulizikutanisha timu hizo mbili, uliochezwa  jana kwenye uwanja wa kisasa  na mkongwe wa Nyamagana, uliokuwa umelenga kujenga mahusiano baina ya chuo hicho na wanahabari.

Habari FC  ilifunga goli kupitia washambuliaji wake  Ramadhani Issa dakika ya 8, Francis Chamungu dakika ya 25 na 80 huku Juma Ayo akiipatia timu hiyo magoli mawili dakika ya 50 na 83, na Open University wakifunga kupitia Benjamin Mwailagila dakika ya 33 na 42, Haji Mwasu dakika ya 17.

Katika kipindi cha kwanza kikosi cha  Habari FC  chini ya Kocha  Balthazar  Mashaka kilionekana kuzidiwa mashambulizi hali iliyopelekea kipindi cha pili  kufanya mabadiliko kwa kuanza   mashambuli  kwa kasi yaliyozaa matunda na kupelekea kuibuka na ushindi huo.

Naye Nahodha wa Habari FC Moses Wiliam alisema, mchezo ulikua mzuri na wapinzani walikua vizuri,hivyo amefurahi  kushinda na kuwaomba wadau wengine ambao wanataka mechi za kirafiki kuja kwani wao wapo tayari.

Pia alisema, baada ya kumaliza mchezo huo wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya kirafiki kahama.
Naye Kaimu Katibj wa  Habari FC Fabian Fanuel alisema, wameshinda japo wamepoteza nafasi ya magoli mengi,hivyo aliwaomba wachezaji kujitokeza kufanya mazoezi sambamba na kuzingatia nidhamu.

Naye Waziri wa Michezo wa  Open University Benjamin Mwailagila alisema, amefurahi na kushukuru timu hiyo kujitokeza na kushiriki pamoja katika mchezo huo, hivyo aliomba ushirikiano huo uendelee.

Kocha wa Habari FC Balthazar Mashaka akitoa maelekezo kwa wachezaji wa timu hiyo Jana katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Openi University, uliochezwa jana katika uwanja wa Nyamagana.

Recommended for you