Michezo

Timu ya Mars Academy yapania Michuano ya Ligi Daraja la Kwanza Mwanza

on

Judith Ferdinand, Mwanza

Timu ya Marsh Academy ya jijini Mwanza imeanza maandalizi  ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa yanayotarajiwa kuanza  hivi karibuni kwenye  uwanja wa Nyamagana.

Hivi  karibuni BMG ilishuhudia wachezaji wa timu hiyo wakifanya  mazoezi katika uwanja wa  Mirongo  wa  jijini  hapa.

Akizungumzia maandalizi  hayo, Mjumbe Kamati  Tendaji  wa timu hiyo Amiry  Musso alisema atahakikisha wanafanya vizuri  katika ligi hiyo kutokana na kauli mbiu  yao ya kufanya  vyema, kwani kikosi  kimejitosheleza kwa ajili ya mashambulizi.

“Katika msimu huu wa 2017/18  tumejiwekea mikakati ya  kufanya vizuri  katika ligi daraja la tatu, kwani siku njema  huonekana  asubuhi  na lengo la mazoezi hayo ni maandalizi  tu, nawaomba   wachezaji kufuata maagizo kutoka  kwa viongozi wao ,”alisema Musso.

Naye Mchezaji wa Timu hiyo, Frank Kulwa alisema atahakikisha anaisaidia timu kufanya vizuri  katika ligi hiyo, ili iweze kupanda daraja.

Kulwa alisema, atafuata maelekezo ya walimu pamoja na kuweka juhudi kwa    kufanya mazoezi binafsi ambayo yatasaidia kufanya vizuri.

Alisema  ni vema kila mchezaji kujiwekea utaratibu wa kufanya mazoezi kila  siku kwani mpira ni ajira kama ilivyo  kazi nyingine   na kwa sasa unalipa tofauti  na  zamani.

Na wakati huo huo Kulwa awaomba wadau na wapenda soka  mbalimbali mkoani hapa,  kujitokeza kuuunga mkono na kusaidia  timu changa ambazo zinawachezaji wenye vipaji, ili waweze kufikia ndoto zao, pamoja na serikali kuhakikisha inatatua changamoto ya viwanja.

Hii ni kutokana na wadau pamoja na serikali kuwekeza na kuangalia timu kubwa ambazo zinawachezaji waliofanikiwa na kusahau wa  chini ambao ndio msingi wa kufanya vizuri katika mchezo huo.

Pia aliwaomba wachezaji wachanga kujitoa katika kushirikj ligi mbalimbali ili kuonyesha vipaji na kuacha kutegemea kupata vitu vikubwa.

Hata hivyo alisema, ili soka la mkoa wa  Mwanza, liendelee ,viongozi,wanachama,wachezaji na wadau wanatakiwa kishirikiana na kuwa wamoja na kuacha majungu, chuki na dharau.

wachezaji wa timu ya marsh Academy wakifanya mazoezi katika uwanja wa Mirogo jijini Mwanza.

Recommended for you