Michezo

Timu ya soka ya Mbao Fc haikamatiki

on

Judith Ferdinand, Mwanza

Timu ya Mbao FC ya jijini Mwanza imewakaribisha Mwadui FC kwa kichapo cha goli 1-0, katika mchezo wa  ligi kuu (VLP) unaondelea nchini.

Katika mchezo huo uliotimua vumbi juzi katika uwanja wa CCM Kirumba, huku Mbao FC wakiwa wenyeji dhidi ya Mwadui FC na kwa mara ya kwanza kushinda mechi kwenye uwanja wa nyumbani tangu kuanza kwa ligi msimu huu.

Katika kipindi cha kwanza  Mbao FC ilifunga goli lililoipa ushindi timu hiyo na kuibuka na pointi tatu kupitia Emmanuel Mvuyekure dakika ya 45.

Akizungumzia mchezo huo Kocha wa  Mbao FC Etiene Ndayiragije alisema,amefurahi kupata matokeo hayo, kwani yamempa ushindi kwa mara ya kwanza akiwa nyumbani tangu kuanza kwa ligi msimu huu.

Pia  alisema, anakikosi cha watu 30, hivyo anapanga kulingana na wapinzani pamoja na mchezaji jinsi anavyo fanya mazoezi na kujitoa,hivyo atakaa na uongozi wa  timu hiyo ili kuona kama watafanya usajili wa  dirisha dogo.

Naye Kocha wa  Mwadui FC Jumanne Ntanbi alisema, mchezo ulikua mgumu,pia walipata nafasi nyingi lakini hawakia makini kuzitumia na wenzao walipata nafasi moja na kuitumia vizuri.

Alisema, wanahitaji nafasi moja ya ushambuliaji na ulinzi katika usajili wa dirisha dogo,kwani vijana wapo vizuri ila hayo ni matokeo.

Recommended for you