Audio & Video

Juhudi za shirika la WoteSawa zaanza kuzaa matunda Jijini Mwanza

on

George Binagi-GB Pazzo, BMG

Wafanyakazi wa nyumbani Jijini Mwanza wamelishukuru shirika la kutetea haki za watoto wafanyakazi wa nyumbani WoteSawa, kwa kuwajengea uwezo wa kujitambua na hivyo kupata haki na stahiki zao kazini.

Baadhi ya wafanyakazi hao wameyasema hayo kwenye kikao baina ya shirika hilo, viongozi wa dini, wenyeviti wa mitaa, watendaji kata, waajiri na wafanyakazi wa nyumbani kilichofanyika Mei 08, 2018 Monach Hotel Manispaa ya Ilemela.

Afisa Program shirika la WoteSwa, Elisha Davis alisema lengo la kikao hicho ilikuwa ni kuweka mikakati ya pamoja ili kuwabaini wafanyakazi wa nyumbani katika Mitaa yao na kuhakikisha wanapata haki na stahiki zao ikiwemo kuwakinga na vitendo vya unyanyasaji na utumikishwaji.

Kikao hicho kiliazimia mikakati kadhaa ikiwemo wenyeviti wa mitaa na watendaji kutumia mikutano ya hadhara kufikisha elimu ya kupinga ukatili kwa wafanyakazi wa nyumbani huku viongozi wa dini nao wakitumia majukwaa yao kufikisha elimu hiyo.

Hii ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa “uwezeshaji shirikishi kwa watoto wafanyakazi wa nyumbani Tanzania” awamu ya kwanza unaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi 2019, unaotekelezwa na shirika la WoteSawa.

Afisa Program, Tathmini na Ufuatiliaji kutoka shirika la WoteSawa, Elisha David akizungumza kwenye kikao hicho.

Kikao hicho kiliazimia mikakati kadhaa ikiwemo wenyeviti wa mitaa na watendaji kutumia mikutano ya hadhara kufikisha elimu ya kupinga ukatili kwa wafanyakazi wa nyumbani huku viongozi wa dini nao wakitumia majukwaa yao kufikisha elimu hiyo.

Mmoja wa washiriki akichangia mada.

Shirika la WoteSawa limekuwa likiwajengea uwezo wadau mbalimbali wakiwemo waajiri wa wafanyakazi wa nyumbani ili kuhakikisha wanatoa mikataba ya kazi kwa wafanyakazi wao kwa manufaa ya pande zote mbili.

Tayari shirika hilo kupitia mradi wa “uwezeshaji shirikishi kwa watoto wafanyakazi wa nyumbani Tanzania” limewafikia wafanyakazi wa nyumbani 150 Jijini Mwanza na kuwajengea uelewa kuhusiana na kazi yao.

Tayari wafanyakazi wa nyumbani 17 Jijini Mwanza wamepewa mafunzo ya salon na hivyo kuwasaidia kujiimarisha kiuchumi.

 

Washiriki wa kikao wakifuatilia kwa umakini kikao hicho.

Waajiri wanahimizwa kuhakikisha wanalinda haki za wafanyakazi wa nyumbani huku wakitakiwa kutowaajiri watoto walio na umri chini ya miaka 14 kwani sheria ya mtoto ya mwaka 2009 inataka mtoto mwenye umri kuanzia miaka 14 ndiye aajiriwe kazi zenye staha zisizoathiri makuzi yake ikiwemo haki ya kupata elimu.

Washiriki wakifurahia jambo kwenye kikao hicho.

Juhudi za shirika la WoteSawa zimeanza kuleta mabadiliko chanya katika jamii kwa katika kulinda na kutetea haki za watoto wafanyakazi wa nyumbani.

Ni wajibu kila mmoja katika jamii kuhakikisha analinda haki za wafanyakazi wa nyumbani.

Ukiona ama kusikia tukio lolote la ukatili kwa mfanyakazi wa nyumbani, toa taarifa mamlaka husika ikiwemo ofisi ya mwenyekiti wa mtaa ama mtendaji.

Wananchi wanahimizwa kutoa taarifa za ukatili na unyanyasi kwa watoto wafanyakazi wa nyumba kwa kupiga simu nambari 0800 71 00 60 bure.

Tazama video hapa chini. 

Bonyeza BMG Habari kwa habari zaidi.

Recommended for you