Audio & Video

Halmashauri ya Misungwi kuanza kampeni ya kutokomeza ukatili wa kijinsia

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Halmashauri ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza inatarajia kuanza kampeni maalum itakayodumu kwa kipindi cha miezi miwili inayolenga kupambana na ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto, wanawake na wazee.

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Eliurd Mwiteleke ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Idara, Maafisa Maendeleo ya Jamii, Watendaji wa Kata na Vijiji, Wenyeviti wa Vijiji, Madiwani, Mahakama, Polisi pamoja na Sungusungu.

Halmashauri ya wilaya ya Misungwi imeandaa mafunzo hayo kwa kushirikiana na shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI ambapo yamefanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Misungwi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa kitaifa wa kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia.

Mkurugenzi Misungwi ambaye pia alikuwa Mwezeshaji kwenye mafunzo hayo

PIA SOMA Shirika la KIVULINI lajizatiti kutokomeza Ukatili wa Kijinsia wilayani Misungwi

Recommended for you