Habari Picha

TUMIA KALENDA YA UTE KUKWEPA MIMBA ZISIZOTARAJIWA. PIA HUSAIDIA KUPANGA MTOTO UMTAKAE.

on

Na:Japhet Kamkono
Kama mzunguko wa mwanamke ni kigeugeu
yaani mwezi huu 28 mara 30 au 32 ama unaenda siku tatu, nne, tano au hata sita kwa vipindi tofauti, basi
itakuwa vigumu kwa mwanamke kukwepa kupata mimba kwa kusoma kalenda.
Njia sahihi ni ya kusoma ute (kipindi cha joto). Ndiyo maana wanyama kama ng’ombe, mbuzi na wengineo, kila
wanapojamiana kinachofuata huwa ni mimba tu, wao hutumia kalenda ya ute wa uzazi.
Kwa mwanadamu kuna aina tatu za
ute muhimu, zikizidi tatu yaweza kukawa na maambukizi.
Ute Wa kwanza ni ute mweupe mzito, huu sio ute wa
uzazi kwa kipindi chochote utakapo onekana. Kwani unazuia mbegu za baba
kulifikia yai. Ute huu huua mbegu za baba ndani ya dakika 30 hivyo aina hii
ya ute haina uzazi.
Ute mwepesi, huu ni ute ambao tunauita “subiri
kidogo” maana yawezekana ukawa umetokana na mihangaiko ya mama
kukasirika, kuchoshwa, kuumwa homa au ikawa ni dalili ya yai kukomaa. Hivyo ukiuona ute huu subiri siku moja uone kama ute utakata au kuongezeka.
Iwapo ute huu
utaendelea kwa Siku mbili hadi tatu jua hapo kuna uzazi. Lakini atakaye tungwa
ni mtoto Wa kike. Hivyo kama lengo ni kukwepa mimba usifanye tendo la ndoa.
Iwapo utapenda mtoto Wa kiume; Subiri kuanzia
hapo kwenye ute mwepesi mpaka “ute unaoteleza kama kiini cha yai”. Ute
huu una uzazi asilimia 98 na unalenga kutungisha mtoto Wa kiume asilimia 99.
Hivyo basi kama wewe siku zako hazigandi, jifunze
kalenda ya ute na itakusaidia kupata mimba kwa kila tendo la ndoa utakalolifanya. Na
itakusaidia kuchagua ni mtoto wa aina gani unamuhitaji.
Kadhalika itakusaidia kukwepa mimba usiyoihitaji. Kalenda ya mzunguko wa tarehe wengi wameshindwa kuitambua vyema kwa sababu ya kubadilika
badilika kwa siku zao zao hedhi kutokana na mikikimikiki ya maisha ambapo iwapo mama
atasafiri safari ndefu tu bila kujali umbali wa safari, siku zake za hedhi zinaweza kuongezeka
au kupungua.

Recommended for you