Audio & Video

Waziri wa Mambo ya Ndani afungua rasmi Mkutano wa Ufunuo wa Matumaini Jijini Mwanza

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Dr.Mwigulu Nchemba amesema serikali itahakikisha uhuru wa taasisi za kidini kufanya shughuli zake ikiwemo ibada unahemishiwa kwani mchango wa taasisi hizo ni mkubwa katika jamii.

Dr.Nchemba alitoa kauli hiyo jana Mei 13, 2018 wakati akifungua rasmi mkutano mkubwa wa injili Ufunuo wa Matumaini (Tumaini la leo, kesho na hata milele), ulioandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Nyanza Kusini katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Awali akisoma risala ya mkutano huo, Katibu Mkuu Kanisa la Waadventista Wasabato Nyanza Kusini, Mchungaji Switta Elias Stevens aliomba serikali kushughulikia suala la waumini wa kanisa hilo kukosa uhuru wa kuabudu kutokana na baadhi ya waajiri kuwapangia kazi siku ya saba ya juma (jumamosi)  huku baadhi wa wanafunzi wakipangiwa kufanya mitihani wakati hiyo ni siku yao ya ibada na wanaoshindwa kutii hutishiwa ama kufukuzwa kazi.

Mkutano wa Ufunuo wa Matumaini (Tumaini la leo, kesho na hata milele) ulianza Mei 12, 2018 na utafikia tamati Juni 02, 2018 ambapo muhubiri mkuu ni Mchungaji Mark Finley kutoka nchini Marekani.

Mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba akizungumza kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Injili wa Ufunuo wa Matumaini (Tumaini la leo, kesho na hata milele). Mhe.Nchemba alifungua rasmi mkutano huo jana Mei 13, 2018 na utafikia tamati Juni 02, 2018 katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Katibu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Nyanza Kusini, Mchungaji Switta Elias Stevens akisoma risala ya mkutano huo.

Mchungaji Mark Walwa Malekana (kulia) akitoa neno la shukurani kwa mgeni rasmi baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano huo ulioanza Mei 12, 2018 katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. Mahubiri na mafundisho ya neno la Mungu yatakuwa yakitolewa kila siku kuanzia saa kumi alasiri hadi saa mbili usiku hadi tamati ya mkutano Juni 02, 2018.

Mchungaji Benard Mwambe akifanya utambulisho wa wageni mbalimbali katika mkutano huo.

Akina mama wa Kanisa la Waadventista Wasabato Nyanza Kusini wakitoa zawadi ya kitenge kwa mgeni rasmi.

Zawadi hii ni maalum kwa Mhe.Nchemba na mkewe.

Mchungaji Mark Finley kutoka Marekani ambaye ni muhubiri mkuu katika mkutano huu wa Ufunuo wa Matumaini.

Mgeni rasmi akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wa dini.

Viongozi mbalimbali wa dini wakiwa pamoja na muhubiri mkuu katika mkutano huu wa Ufunuo wa Matumaini, Mchungaji Mark Finley kutoka Marekani.

Mhe.Nchemba pamoja na viongozi mbalimbali wa dini wakifuatilia matukio kwenye uzinduzi wa mkutano huo.

Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba akishuhudia halaiki ya watoto na vijana kutoka Kanisa la Waadventista Wasabato Nyanza Kusini.

Waziri Nchemba akishuhudia halaiki ya akina mama wa kanisa la Waadventista Wasabato waliokuwa wakiongozwa na Mama Kazi (mwenye kinasa sauti).

Akina mama wakitoa salamu kwa mgeni rasmi.

Halaiki ya akina mama ikipita mbele ya mgeni rasmi kwa mwendo wa kikakamavu.

Viongozi mbalimbali wakifuatilia matukio ya ufunguzi wa mkutano huo.

Muhubiri mkuu Mchungaji Mark Finley kutoka Marekani pamoja na viongozi mbalimbali wakishuhudia ufunguzi huo.

Mgeni rasmi akishuhudia matukio mbalimbali kwenye ufunguzi huo.

Umati wa wananchi na waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabati wakishuhudia matukio mbalimbali kwenye ufunguzi wa mkutano huo.

Viongozi mbalimbali wa dini wakishuhudia ufunguzi wa mkutano huo.

Ufunguzi huo ulikuwa wa kuvutia.

Viongozi mbalimbali wa dini wakishuhudia ufunguzi wa mkutano huo.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Mara Samwel Kiboye (Namba Tatu) ambaye pia ni muumini mzuri wa kanisa la Waadventista Wasabato akisalimiana na Amicus Butunga wa Dira Media.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Mara Samwel Kiboye maarufu kama Namba Tatu (kushoto), akiteta jambo na kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wasabato.

Viongozi mbalimbali kwenye mkutano huo akiwemo Mkuu wa TAKUKURU mkoani Mwanza Ernest Makale (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Mara Samwel Kiboye maarufu kama Namba Tatu (katikati).

Wanakwaya kutoka Kanisa la Wasabato Nyanza Kusini.

Wanakwaya kutoka Kanisa la Wasabato Nyanza Kusini.

Wanakwaya kutoka kanisa la Wasabato.

Tunafuatilia mkutano wa Ufunuo wa Matumaini.

Mgeni rasmi Mhe.Dr.Mwigulu Nchemba (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Kanisa la Wasabato Afrika Mashariki na Kati Dr.Blasios Kaguri (kulia) kutoka Nairobi nchini Kenya.

Mshereheshaji Mtangazaji Maduhu kutoka Morning Star redio na TV kwenye mkutano huo.

 

Tazama Video hapa chini.  

Kanisa la Waadventista Wasabato laandaa Mkutano Mkubwa wa Injili Mwanza

Recommended for you