Audio & Video

UMISSETA: Waziri Mkuu atoa maelekezo kufufua michezo nchini

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amesema hali ya kiwango cha michezo nchini si ya kuridhisha hivyo lazima wanamichezo kuanzia shule za awali, msingi, sekondari pamoja na vyuo waandaliwe vyema.

Waziri Majaliwa aliyasema hayo jana katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza wakati akifungua rasmi Mashindano ya Umoja wa Michezo kwa shule za Sekondari nchini UMISSETA, ulioambatana na pia na ufunguzi wa mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa shule za Msingi UMITASHUMTA.

Ili kuinua kiwango cha michezo nchini, Waziri Majaliwa alisema ni vyema waalimu wakaendelea kuvitumia vyema vipindi vya michezo mashuleni na kuwajengea wanamichezo uelewa mpana kwa kuwatumia waalimu wa michezo wenye taaluma hiyo.

Aidha Waziri Majaliwa aliwataka wasimamizi wa mashindano ya UMISSETA kuhakikisha wanatoa fursa kwa wanafunzi kushiriki mashindano hayo na kwamba hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa kwa mkoa utakashirikisha wachezaji mamluki (wasio wanafunzi).

Aliagiza mikoa na wilaya zote nchini kuhakikisha masomo ya Haiba, Michezo na Stadi za Kazi kwa shule za Msingi pamoja na Elimu ya Michezo kwa shule za Sekondari yanafundishwa kikamilifu, Vyuo vya Elimu ya Michezo vikiwaendeleza waalimu wa michezo huku wanafunzi wakishiriki mchaka mchaka kila siku asubuhi kabla ya vipindi vya darasani.

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza alisema wizara hiyo iko kwenye mchakato wa kuhakikisha sera ya michezo ya mwaka 1995 inahuishwa (inaboreshwa) ili kuendana na mazingira halisi ya michezo nchini.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Elisante Ole Gabriel alisema mashindano ya UMISSETA mwaka huu yanashirikisha wanamichezo 3,680 kutoka mikoa 28 nchini huku UMITASHMTA yakirikisha wanamichezo 3,172 ambapo lengo kuu ni kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana kupitia michezo mashuleni.

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella alitoa pongezi kwa viongozi na wadau wote wakiwemo wadhamini wakuu kampuni ya Cocacola kwa kufanikisha maandalizi ya michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA inayofanyika kwa mwaka wa tatu mfululizo Jijini Mwanza ambapo mwakani michezo hiyo itafanyika Jijini Dodoma.

Nao baadhi ya washiriki wa michezo hiyo waliahidi kuitumia vyema kwa kuonyesha ushindani mkali na kwa nidhamu kwani hiyo ni hatua muhimu ya kuonyesha vipaji vyao na hatimaye kusonga mbele ikiwemo kupata fursa ya kuchezea timu za taifa.

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza kwenye ufunguzi huo.

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akizungumza kwenye ufunguzi huo

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza kwenye ufunguzi wa mashindano hayo

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella akitoa salamu zake kwenye ufunguzi wa mashindano hayo

Mwakilishi kutoka kampuni ya Nyanza Botlling inayozalisha vinywaji jamii ya Cocacola ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano hayo akiwasilisha salamu zake

Baadhi ya washiriki

Ufunguzi wa mashindano ya UMISSETA upande wa soka, pembe Waziri Mkuu Majaliwa akishuhudia

Go Goo Gooo Goooo

Tazama BMG Online TV hapa chini 

SOMA Mapokezi ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Jijini Mwanza

Recommended for you