Audio & Video

Wadau wa mazingira mkoani Mwanza wakutana kuweka mikakati ya LVEMP III

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Wadau wa usafi wa mazingira mkoani Mwanza wamehimizwa kuwashirikisha ipasavyo wananchi katika suala la utunzaji wa mazingira ili kuondokana na hatari zitokanazo na uharibifu wa mazingira.

Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella ametoa rai hiyo leo wakati akifungua kikao cha wadau wa mazingira mkoani Mwanza, kilichoshirikisha wadau mbalimbali wa mazingira ikiwemo NEMC, MWAUASA na halmashauri.

Mbali na kusimamia sheria ipasavyo, Mongella amesema ni vyema wananchi na viongozi wenye ushawishi katika jamii wakiwemo wanasiasa, viongozi wa dini pamoja na mitaa wakajengewa uwezo zaidi ili kushiriki ipasavyo kwenye uhifadhi wa mazingira.

Mratibu wa Uhifadhi wa Mazingira ya Ziwa Victoria LVEMP, Omary Myanza amesema wadau hao wa usafi wa mazingira mkoani Mwanza wameshirikishwa kwenye kikao hicho ili kwa pamoja kujadili na kuandaa mikakati itakayosaidia utekelezaji wa mradi LVEMP III unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella akifungua kikao cha wadau wa mazingira kilichofanyika hii leo Jijini Mwanza. Kushoto ni Mratibu wa Mradi wa Uhifadhi wa Mazingira ya Ziwa Victoria LVEMP nchini Tanzania, Omary Myanza. Mradi wa LVEMP awamu ya kwanza ulianza utekelezaji wake mwanza 1997 hadi 2009, awamu ya pili mwaka 2009 hadi Disemba 2017 na awamu ya tatu inatarajiwa kuanza hivi karibuni ikitekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano.Mtaalam wa hifadhi ya udongo na maji katika mradi wa LVEMP, Nesphory Subira akifafanua jambo kwenye kikao hicho.Baadhi ya washiriki wa kikao hicho kilichoshirikisha wadau mbalimbali wa mazingira ikiwemo NEMC, MWAUASA na halmashauri.

Wadau wakifuatilia kikao hicho.Wadau wa mazingira mkoani Mwanza wakifuatilia kikao hicho.

Tazama BMG Online TV hapa chini 

SOMA TBL MWANZA WAFANYA USAFI MTO MIRONGO

Recommended for you