Habari Picha

Harambee ujenzi wa kituo cha watoto yatima wilayani Tarime

on

Wananchi katika wilaya ya Tarime mkoani Mara wakiwa kwenye tamasha la changizo kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kulelea watoto yatima kiitwacho “Yatima Band”.

Na Frankius Cleophace, Tarime

Ili kukabiliana na changamoto ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu kukimbilia mitaa katika wilaya ya Tarime, Kanisa la Free Pentecost Church Tanzania (FPCT) wilayani hapa limeendesha harambee kwa ajili ya upatikanaji wa shilingi milioni 200 ili kuanza ujenzi kituo hicho.

Katika harambee hiyo iliyofanyika kwenye uwanja wa Serengeti Mjini Tarime, shilingili milioni mbili na laki nne pamoja na tripu 10 za mchanga zilipatikana ambapo mgeni rasmi Michale Kembaki ambaye ni mdau wa maendeleo alichangia shilingi milioni mbili.

Magesa Patrick ambaye ni mmoja  wa wajumbe wa kituo hicho kiitwacho “Yatima Band” alisema kuanza na kukamilika kwake kutasaidia kutoa malezi bora kwa watoto yatima badala ya kukimbilia mtaani hivyo wanajamii wanapaswa kutoa ushirikiano wao.

Mgeni rasmi, Michael Kembaki akizungumza kwenye tamasha hilo. Kembaki ni dau wa maendelo ambapo mwaka 2015 aliwania nafasi ya ubunge jimbo la Tarime Mjini (CCM)

Viongozi mbalimbali kwenye tamasha hilo lililofanyika uwanja wa Serengeti (Shamba la Bibi) Mjini Tarime

Recommended for you