Audio & Video

ILEMELA: Mkandarasi asaini mkataba ujenzi wa barabara ya Sabasaba-Kiseke-Buswelu

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza imesaini mkataba na kampuni ya Sinohydro Corporation kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Sabasaba-Kiseke Buswelu yenye urefu wa kilomita 9.7 kwa kiwango cha lami.

Hafla ya utilianaji saini mkataba huo imefanyika leo katika Kata ya Kiseke ambapo Mkurugenzi wa Manispaa hiyo John Wanga amesema gharama za ujenzi huo ni zaidi ya shilingi bilioni 18 na umepangwa kukamilika ndani ya miezi 15.

Aidha amesema mkataba huo pia utahusisha ujenzi wa barabara ya Isamilo-Mji Mwema-Big Byte yenye urefu wa kilomita 1.2 na barabara ya Makongoro-Mwaloni-Kigoto yenye urefu wa kilomita 1.2 ambapo mkataba huo unahusisha uwekaji wa taa za barabarani pamoja na mabirika ya kukusanyia taka.

Mwakilishi wa kampuni ya Sinohydro kutoka nchini China inayojenga barabara hiyo, Jia Bin ameahidi kutekeleza mradi huo kwa wakati na kwa ubora ubora huku akiahidi kutoa kipaumbele cha ajira za muda mfupi kwa wenyeji.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Renatus Mulunga amesema tayari Manispaa hiyo imelipa fidia ya shilingi Milioni 436 kati ya shilingi Milioni 636 ili kupisha utekelezaji wa mradi huo.

Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Ilemela wakiwemo bodaboda na Mama Lishe wametoa pongezi kwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa kutekeleza ahadi ya kujenga barabara ya Sabasaba-Kiseke-Buswelu kwa kiwango cha lami na kwamba itawarahisishia shughuli zao za uzalishaji mali.

Mkurugenzi Manispaa ya Ilemele John Wanga (kulia), Mstahiki Meya Manispaa hiyo Renatus Muluna (wa pili kulia), Youn Kai (wa pili kushoto) pamoja na Jia Bin (kushoto) kutoka kampuni ya Sinohydro wakisaini mkataba huo.

Kutoka kushoto ni Youn Kai, Jia Bin, kutoka kampuni ya Sinohydro pamoja na Mstahiki Meya Manispaa ya Ilemela wakisaini mkataba wa ujenzi wa barabara ya Sabasaba-Kiseke-Buswelu.

Kutoka kushoto ni Youn Kai, Jia Bin, kutoka kampuni ya Sinohydro pamoja na Mstahiki Meya Manispaa ya Ilemela Renatus Mulunga pamoja na Mkurugenzi Manispaa hiyo John Wanga wakisaini mkataba wa ujenzi wa barabara ya Sabasaba-Kiseke-Buswelu.

Mkataba wa makubaliano kwa ajili ya ujenzi huo.

Ujenzi huo utarahisisha huduma ya usafiri kwa wakazi wa Manispaa ya Ilemela

Pongezi baada ya mkataba kusainiwa

Wakazi wa Ilemela wamefurahishwa na hatua hii na kuomba mradi ukamilike kwa wakati

Kutoka kushoto ni mwakilishi wa kampuni ya Sinohydro Corporation Jia Bin, Mstahiki Meya Manispaa ya Ilemela Renatus Mulunga pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo John Wanga wakionyesha mkataba wa makubaliano.

Tazama BMG Online TV hapa chini 

SOMA Baraza la Madiwani kuhusu barabara Buswelu-Sabasaba

Recommended for you