Audio & Video

Jiji la Mwanza lasaini mkataba ujenzi wa dampo la kisasa na barabara za lami

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Halmashauri ya Jiji la Mwanza imesaini mkataba na kampuni ya Nyanza Road Works kwa ajili ya ujenzi wa barabara za lami pamoja na dampo la kisasa.

Akizungumza jana kwenye zoezi la utilianaji saini mkataba huo, Kaimu Mkurugenzi Jiji la Mwanza Philipo Mkama alisema barabara zitakazojengwa ni Mtakuja, Sukuma, Umoja, Machemba, Pamba B, Bomba, Lumumba zenye urefu wa kilomita 4.4 pamoja na dampo la kisasa la Buhongwa, ambapo kataba huo unagharimu shilingi bilioni 15.9 kupitia ufadhili wa Benki ya Dunia.

Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa ahadi kwa wananchi na kwamba ujenzi wa barabara hizo utasaidia kuondoa changamoto ya ubovu wa barabara Jijini Mwanza huku dampo la kisasa Buhongwa likiimarisha uwezo wa halmashauri kukusanya taka tofauti na ilivyo sasa.

Zoezi la utilianaji saini mkataba huo lilifanyika ukumbi wa halmashauri ya Jiji la Mwanza na kushuhudiwa na Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Marry Tesha ambapo alisisitiza mkandarasi kutekeleza mradi kwa kiwango ndani ya kipindi cha miezi 15 cha mkataba huo.

na Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Marry Tesha akizungumza wakati wa zoezi la utilianaji saini mkataba huo baina ya halmashauri ya Jiji la Mwanza na mkandarasi kampuni ya Nyanza Road Works

Mstahiki Meya Jiji la Mwanza, James Bwire akizungumza wakati wa zoezi hilo

Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula akiwasilisha salamu zake

Mkurugenzi Jiji la Mwanza Kiomoni Kibamba akisaini mkataba ujenzi wa barabara za lami na dampo la kisasa

Mstahiki Meya Jiji la Mwanza, James Bwire (kushoto) na Mkurugenzi Jiji la Mwanza Kiomoni Kibamba (kulia) wakisaini mkataba huo

Kutoka kushoto ni Mhandisi Vishal Patel kutoka kampuni ya Nyanza, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Ainash Patel na Mstahiki Meya Jiji la Mwanza, James Bwire wakisaini mkataba huo

Kutoka kushoto ni Mhandisi Vishal Patel kutoka kampuni ya Nyanza, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Ainash Patel na Mstahiki Meya Jiji la Mwanza, James Bwire wakisaini mkataba huo

Mkurugenzi kampuni ya Nyanza (kushoto) akipokea mkataba wa ujenzi wa barabara za lami Jijini Mwanza na dampo la kisasa Buhongwa kutoka kwa Mstahiki Meya Jiji la Mwanza

Watendaji mbalimbali Jijini Mwanza wakishuhudia zoezi hilo

Tazama BMG Online TV hapa chini 

SOMA ILEMELA: Mkandarasi asaini mkataba ujenzi wa barabara ya Sabasaba-Kiseke-Buswelu

Recommended for you