Audio & Video

Alichobaini RC Mongella baada ya kukagua maghala ya sukari na Mafuta

on

George Binagi-GB Pazzo, BMG

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella leo jumamosi Mei 12, 2018 amefanya ukaguzi wa maghala ya sukari na mafuta ya kula Jijini Mwanza, ili kujionea hali halisi ikiwa imesalia wiki moja kabla ya waumini wa dini ya kiislamu kuanza mfungo wa Ramadhan.

Pamoja na mambo mengine aliyoyabaini katika ukaguzi huo, Mhe.Mongella pia ametoa tahadhari kwa wafanyabiashara kuwa waadilifu na kutojihusisha na upandishaji wa bidhaa mbalimbali kwa kigenzo cha mfungo wa mwezi Ramadhan na kwamba watakaokiuka, hatua zitachukuliwa dhidi yao.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella akikagua akiba ya sukari katika ghala la kiwanda cha Kagera Sugar lililopo eneo la Igogo Jijini Mwanza. Pembeni ni Mkurugenzi wa kampuni ya V.H Shah.

Shehena ya sukari katika ghala la kampuni ya V.H Shah.

Hali ya akina ya upatikanaji wa sukari mkoani Mwanza imeonekana kuridhisha.

Shehena ya sukari katika ghala la kampuni ya V.H Shah.

Ukaguzi wa shehena ya sukari Jijini Mwanza.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella (kulia), akizungumza na meneja wa kampuni ya Mohamed Enterprises Roshan Ali alipofanya ukaguzi kwenye maghala yake ya sukari na mafuta.

Meneja wa kampuni ya Mohamed Enterprises Roshan Ali amemhakikishia RC Mongella kuhusu uingizaji zaidi wa mafuta ya kula na hivyo kukidhi mahitaji yalipo mkoani Mwanza na mikoa jirani.

Ukaguzi wa sukari na mafuta ya kula katika ghala la kampuni ya Mohamed Enterprises Jijini Mwanza.

RC Mongella akipokea ufafanuzi kuhusu hali ya upatikanaji wa sukari na mafuta ya kula.

Wafanyabiashara mkoani Mwanza wametakiwa kutopandisha bei ya bidhaa mbalimbali kuelekea mfungo wa mwezi Ramadhan.

Tazama video kamili hapa chini. 

Fungua BMG Habari kwa taarifa zaidi.

Recommended for you