Audio & Video

MWANZA: Machinga walio barabarani watakiwa kuondoka kwa hiari

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella amekagua ukarabati wa barabara ya Pamba kwa kiwango cha lami Jijini Mwanza na kuridhishwa na ukarabati huo unaotekelezwa na kampuni ya Nyanza Road Works kwa gharama ya shilingi bilioni 1.4.

Mhe.Mongella alifanya ukaguzi huo jana akiambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa wilaya Nyamagana Mhe.Marry Tesha Onesmo, Viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza pamoja na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini TARURA unaosimamia barabara hiyo.

Akiwa katika ziara hiyo, Mhe.Mongella alisikitishwa na baadhi ya wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) ambao alikuta wamepanga bidhaa zao katika hifadhi ya barabara na hivyo kuwataka waondoe bidhaa hizo kwenye hifadhi ya barabara kwani ni hatari kwao kiusalama na pia zinasababisha zinasababisha adha kubwa hususani kwa watembeaji wa miguu.

Ukarabati wa barabara ya Pamba umefikia katika hatua za mwisho na itafunguliwa muda wowote kuanzia leo na kuondoa adha iliyokuwepo hapo awali.

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella (mwenye kofia), akisikiliza ufafanuzi kutoka TARURA kuhusu ukarabati wa barabara ya Pamba.

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella akisalimiana na mmoja wa Machinga ambaye ni mlemavu wa miguu katika eneo la barabara ya Pamba Jijini Mwanza

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella akiteta jambo na viongozi wa Umoja wa Machinga mkoani Mwanza (kulia)

SOMA TARURA wasikia kilio cha watumiaji wa barabara mkoani Mwanza

Recommended for you