Audio & Video

“Ukisikia ama kushuhudia vitendo vya Ukatili toa taarifa”- KIVULINI

on

BMG Habari-Pamoja Daima!

Ni katika shule ya sekondari Sanjo iliyopo Kata ya Usagara wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, ikiwa huu ni mwendelezo wa midahalo inayoendeshwa na Shirika la Kutetea Haki za Wasichana na Wanawake KIVULINI lililopo Nyamhongolo Jijini Mwanza.

Shirika hili linaendesha midalaho hii katika shule kadhaa za sekondari kutoka Kata 10 za wilaya ya Misungwi, ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa miaka mitano wa Kuhamasisha na Kuijengea Uwezo Jamii ili Kupinga Vitendo vya Ukatili dhidi ya Wasichana na Wanawake.

Hapa wanafunzi wanaelezwa bayana kwamba ukatili ni maneno ama matendo anayotendewa mtu yeyote na ukatili huu unagawanyika katika nyanja kuu nne ambazo ni ukatili wa kimwili, kisaikolojia, kingono na kiuchumi ambapo wahanga wakubwa katika jamii ni watoto na wanawake.

Wanafunzi wanajengewa uwezo wa kutambua na kufichua aina zote za ukatili mashuleni na majumbani, lengo ni kuwa na jamii salama isiyo na ukatili ambapo elimu wanayoipata hapa wataitumia kuwaelimisha wananzengo wengine huku nao pia ikiwasaidia katika maisha yao kwani nao ni wazazi na walezi wa baadaye.

Tayari midahalo hii imefanyika katika shule za sekondari Sanjo, Igokelo, Idetemya, Misasi, Mawe Matatu, Misungwi pamoja na Koromije na sasa wanafunzi wa shule hizi ni mabalozi wazuri wa mapambano dhidi ya ukatili katika jamii.

Bonyeza HAPA kusoma habari nyingine.

Recommended for you