Audio & Video

Ukweli kuhusu fedha za ujenzi wa meli mpya Ziwa Victoria

on

Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) imeingiamikataba mine ambayo ni ujenzi wa meli mpya nay a kisasa katika Ziwa Victoria, chelezo na ukarabati wa meli za Mv. Victoria na Mv. Butiama na kampuni kutoka Jamhuri ya Korea Kusini wenye thamani ya shilingi bilioni 152.

Meli hiyo mpya ya abiria na mizigo itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200, tani 400 za mizigo na magari madogo 20 ambapo mkandarasi ni M/S Gas Entec Company Limited ya Korea Kusini akishirikiana na SUMA JKT kutoka Tanzania na kampuni ya KANGNAM Corporstion ya Korea Kusini pia kwa gharama ya shilingi bilioni 88.764 na unatarajiwa kukamilika kwa muda wa miaka miwili.

Aidha ujenzi wa chelezo itakayotumika kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya utatekelezwa na mkandarasi M/S STX Engine Company Limited akishirikiana na kampuni ya SAEKYUNG Construction Company Limited zote kutoka Korea Kusini kwa gharama ya shilingi bilioni 35.994 na ujenzi huo utachukua muda wa mwaka mmoja.

Pia ukarabati wa meli za Mv. Victoria na Mv. Butiama utatekelezwa na kampuni ya KTMI Co.LTD ya Korea Kusini ikishirikiana na kampuni ya YUKO’S Enterprises (EA) Co.Ltd kwa gharama za shilingi bilioni 27,009,738,200 ambapo shilingi bilioni 22,712,098,200 ni kwa ajili ya ukarabati wa meli ya Mv. Victoria na shilingi bilioni 4,897,640,000 ni kwa ajili ya ukarabati wa meli ya Mv. Butiama.

Akizungumza baada ya kushuhudia zoezi la utilianaji saini mikataba hiyo, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alielezea chanzo cha fedha hizo.

Balozi wa Korea Kusini hapa nchini Song Geum Yong akizungumza kwenye hafla hiyo
Mikataba iliyosainiwa leo
Tazama hapa chini BMG Online Tv

Recommended for you