Audio & Video

Mashindano ya UMISETA mkoani Mwanza yaanza kwa kishindo

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Mashindano ya umoja wa michezo, sanaa na taaluma yanayoshirikisha shule za sekondari nchini UMISETA yameanza hii hii leo katika ngazi ya mkoa wa Mwanza kwa kushirikisha zaidi ya washiriki mia tisa kutoka halmashauri zote nane.

Akifungua mashindano hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mkuu wa wilaya Magu Khadija Nyembo amewataka washiriki kuwa waadilifu na kujiepusha na vitendo viovu vinavyoweza kukatisha ndoto zao hususani kujiepusha na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Afisa Elimu mkoani Mwanza Mw.Michael Ligola amesema mashindano hayo yamekuwa chachu ya kuibua vipaji vya michezo mbalimbali ikiwemo soka ambapo mwaka jana mkoa wa Mwanza ulishika nafasi ya pili UMISETA kitaifa na nafasi ya kwanza UMITASHUMIKA kitaifa hivyo mwaka huu ushindani unatarajiwa kuwa mkubwa zaidi.

Afisa Michezo mkoani Mwanza James Willium Ngassa amebainisha kwamba mwaka huu ni mara ya nne mashindano ya UMISETA na UMITASHUMITA kufanyika mkoani Mwanza kitaifa ambapo mashindano ya UMISETA kitaifa yanatarajiwa kuanza Juni 04 hadi 15, 2018 na UMITASHUMITA ni kuanzia Juni 17 hadi 29, 2018 katika vituo vya chuo cha elimu Butimba na Nsumba sekondari Jijini Mwanza na kwamba uzinduzi utafanyika Juni 05, 2018 katika uwanja wa CCM Kirumba.

Baadhi ya washiriki wa mashindano ya UMISETA ngazi ya mkoa wa Mwanza yanayofanyika katika shule ya sekondari Nsumba Jijini Mwanza, wamejinasibu kujiandaa vyema ili kuhakikisha wanaleta changamoto kiushindani katika mashindano ya UMISETA kitaifa.

Mkuu wa wilaya Magu Mhe.Khadija Nyembo akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza kwenye ufunguzi wa mashindano ya UMISETA ngazi ya mkoa Mwanza.

Mkuu wa wilaya Nyamagana mkoani Mwanza akizungumza kwenye uzinduzi wa mashindano hayo.

Mkuu shule ya sekondari Nsumba akitoa neno la shukurani kwa niaba ya umoja wa wakuu wa shule za sekondari mkoani Mwanza.

Wakuu wa elimu kutoka halmashauri mbalimbali mkoani Mwanza.

Washiriki kutoka halmashauri ya Jiji la Mwanza.

Washiriki kutoka halmashauri ya wilaya Kwimba.

Washiriki kutoka halmashauri ya wilaya Misungwi.

Washiriki kutoka halmashauri ya wilaya Ukerewe.

Washiriki kutoka halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema.

Washiriki kutoka halmashauri ya wilaya Magu.

Washiriki kutoka halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.

Washiriki kutoka halmashauri ya wilaya ya Sengerema.

Washiriki wakifurahia ufunguzi wa mashindano ya UMISETA mkoani Mwanza.

Tazama video hapa chini. 

ISOME PIA HABARI HII MWANZA WABANWA BAADA YA KUNG’ARA UMITASHUMITA NA UMISETA

Recommended for you