Michezo

Ushindani mkali mashindano ya UMISETA kitaifa Jijini Mwanza

on

Judith Ferdinand, BMG

Mashindano ya michezo kwa shule za sekondari nchini UMISETA ngazi ya Taifa yameanza kutimua vumbi rasmi June 4, 2018 Jijini Mwanza ambapo viongozi wa mikoa shiriki wametahadharishwa kuwajumuisha wachezaji wasio na vigezo (mamluki).

Akizungumza katika ufunguzi wa mashindano hayo, Mwenyekiti wa UMISETA Taifa Leonard Thadeo alisema mkoa utakaochezesha wachezaji mamluki watawafukuza pamoja na viongozi kusimamishwa kushiriki katika mashindano hayo kwa miaka mitano.

“Hatutakuwa tayari kuona ratiba au michezo inavurugwa kwani serikali imetumia gharama kubwa kuiandaa hivyo taratibu na kanuni zifuatwe”. lisema Thadeo.

Kwa upande wake Katibu UMISETA Taifa, Aaron Sokoni alisema mashindano hayo yanafanyika mkoani Mwanza kwa ngazi ya taifa ambayo yanatimua vumbi katika viwanja viwili vya Chuo cha Ualimu Butimba na shule ya Sekondari Nsumba yakishirikisha wanamichezo 3360.

Michezo mbalimbali ilifanyika ambapo kwa upande wa soka wavulana Geita walishinda wapinzani wao Ruvuma kwa goli 3-1, Njombe na Mara wakitoka suluhu ya bila kufungana, Morogoro dhidi ya Manyara walitoka sare ya goli 1-1 huku Lindi ikiibuka kidedea dhidi ya Kigoma kwa goli 4-1.

Katika mchezo wa kikapu Dar es salaam imeilaza Lindi kwa goli 67-11 huku Morogoro ikitoakichapo cha goli 62-22 dhidi ya Mara.

Upande wa mpira wa pete Dar es salaam imeifunga Geita goli 47-11, Kigoma ikitoa kichapo cha goli 32-19 dhidi ya Kilimanjaro, Morogoro imetoa dozi ya goli 38-14 huku Dodoma wakipata ushindi wa mezani wa goli 40 baada ya wapinzani wao Pemba kutoshiriki.

Katika mchezo wa mpira wa mikono wavulana Mbeya iliilaza chali Geita kwa goli 21-17 huku Tanga wakiifunga Shinyanga goli 35-20. Kwa upande wa wasichana Mara waliifunga Njombe goli 8-4 na Kigoma ikitoa kichapo cha goli 9-5 dhidi ya Lindi.

TAZAMA Mashindano ya UMISETA mkoani Mwanza yaanza kwa kishindo

Recommended for you