Michezo

Mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya wilaya Ilemela yaibua vipaji zaidi

on

Meneja Mauzo na Masoko kutoka kampuni ya Fide Investements inayozalisha maji ya Mwanza, Deus Daud akimkabidhi kombe mwakilishi wa Kanda ya Bugogwa baada ya kuibuka mshindi kipengere cha riadha.

Judith Ferdinand, BMG

Kanda ya Bugogwa imeibuka kinara katika mashindano ya michezo kwa shule za msingi UMITASHUMTA ngazi ya wilaya ya Ilemela mkoani yaliyofikia tamati Juni 02, 2018 katika uwanja wa shule ya sekondari ya wavulaa Bwiru iliyopo Manispaa ya Ilemema mkoani Mwanza.

Kanda hiyo katika michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu kwa wasichana, mpira wa mikono kwa wasichana na wavulana, mpira wa pete, mpira wa wavu wasichana na wavulana, riadha na mshindi wa jumla wa mashindano hayo.

Mmoja wa washiriki kutoka Kanda ya Bugogwa, Elis Rodges alisema siri ya ushindi ni mazoezi pamoja na kuandaliwa vizuri na walimu wao kuanzia ngazi ya shule ambapo aliwaomba waandaaji kuendelea kuboresha mashindano hayo huku akiahidi kufanya vizuri katika mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya mkoa.

Naye Msimamizi wa Kanda ya Bugogwa, Omary Ibrahim alisema kufurahishwa na ushindi wa vikombe vinane na kwamba halmashauri ya Manispaa ya Ilemela inatarajia kutoa vipaji zaidi kupitia mashindano hayo.

Mratibu wa Michezo Ngazi ya Wilaya ya Ilemela, Deogratias Sollo alisema lengo la mashindano hayo ni kuibua na kuendelea vipaji mbalimbali mashuleni, taaluma kwa wanafunzi, kudumisha undugu, urafiki na afya ambapo alibainisha kwamba licha ya mashindano hayo kufanikiwa bado wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vifaa vya vichezo ikiwemo sare kwa wanafunzi na waalimu.

Meneja Mauzo na Masoko wa kampuni ya Fide Investments Co.Ltd, Deus Daud ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa mashindano hayo alisema michezo ni ajira, furaha na afya hivyo kampuni hiyo inaunga mkono juhudi za serikali katika kuendeleza michezo kwa vijana ambapo itasaidia kutatua baadhi ya changamoto ili kuboresha mashindano hayo ngazi ya mkoa.

Hata hivyo Afisa Michezo Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Bahati Kizito alisema mashindano hayo yalimalizika vyema ambapo wamechuja wachezaji 120 wanakaoshiriki mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya mkoa yanayotarajiwa kuanza Juni 06, 2018 katika viwanja vya shule ya wavulana Bwiru.

Meneja kampuni ya Fide Investments, Vimal Singh (kushoto) akimkabidhi kombe mwakilishi wa Kanda ya Bugogwa baada ya kuibuka mshindi na ushindi.

Afisa Michezo Manispaa ya Ilemela, Bahati Kizito akizungumza kwenye kilele cha UMITASHUMTA wilayani Ilemela.

Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ilemela, Mwl.Marco Busungu akizungumza kwenye ufungaji wa mashindano hayo.

Meneja Mauzo na Masoko kutoka kampuni ya Fide Investements inayozalisha maji ya Mwanza, Deus Daud akizungumza kwenye kilele cha mashindano hayo.

Viongozi mbalimbali wakiimba wimbo wa Taifa. Tazama HAPA UMISETA ngazi ya mkoa Mwanza.

Recommended for you