Audio & Video

Mashindano ya UMITASHUMITA yapamba moto mkoani Mwanza

on

Judith Ferdinand, BMG

Mashindano ya michezo kwa shule za msingi UMITASHUMTA ngazi ya mkoa wa Mwanza yameendelea kutimua vumbi tangu Juni 06, 2018 katika viwanja vya shule ya wavulana Bwiru wilayani Ilemela.

Mashindano hayo yanashirikisha timu kutoka halmashauri zote nane za mkoani Mwanza ambapo michezo mbalimbali  inaendelea kupamba moto ikiwemo soka, wavu, riadha kwa wavulana na wasichana, pete pamoja na kikapu.

Mratibu wa UMITASHUMTA mkoani Mwanza, Joseph Mambo anasema mashindano hayo yameanza vyema na kila timu inaonyesha mkubwa hivyo matumaini ni kupata timu bora ya mkoa ambayo itawakilisha vizuri ngazi ya taifa.

Mambo alisema mashindano hayo yatafikia tamati kesho Juni 10 huku akitumia fursa hiyo kuwataka wakazi wa Mwanza kujitokeza kwa wingi hii leo ambayo itakuwa ni kwa ajili ya fani za ndani ikiwemo ngoma,ngonjera, mashairi ili kupata burudani na kushuhudia vipaji vya watoto.

Siku ya pili ya mashindano hayo matokeo kwa upande wa soka wavulana yalikuwa, halmashauri ya Sengerema 2-0 Kwimba, Magu 0-1 Ilemela huku wasichana Magu 3-2 Misungwi, Kwimba 1-0 Ukerewe na Ilemela 0-1 Buchosa.

Aidha mchezo wa wavu wavulana Kwimba 2-0 Ukerewe, Nyamagana 0-2 Magu, Buchosa 2-1 Misungwi na Sengerema 2-1 Ukerewe huku wasichana Sengarema 2-0 Buchosa.

Vilevile katika mchezo wa pete Nyamagana 18-28 Buchosa, Ukerewe 4-41 Buchosa, Ilemela 32-10 Magu,Kwimba 8-26 Sengerema na Misungwi 41-3 Ukerewe.

SOMA Mashindano ya UMISETA mkoani Mwanza yaanza kwa kishindo 

Recommended for you