Audio & Video

Wananchi wafunguka upanuzi wa Kituo cha Afya Koromije Misungwi

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Wananchi wamepokea kwa furaha hatua ya serikali kutoa pesa kwa ajili ya upanuzi wa Kituo cha Afya Koromije kilichopo Misungwi mkoani Mwanza wakisema itawaondolea adha ya usumbufu wa kufuata huduma za afya umbali mrefu.

Baadhi ya wakazi wa Koromije, Mwanne Omary pamoja na Shinji Maduka wanasema walikuwa wakipata adha ya ukosefu wa chumba cha kuhifadhia maiti, wodi ya wazazi, upasuaji pamoja na maabara hivyo hatua ya serikali kutoka pesa kwa ajili ya ujenzi wa huduma hizo wameipokea kwa furaha na kuahidi kutoa ushirikiano wao kupitia nguvu kazi.

Mganga Mfawidhi kituo cha Afya Koromije, Dr.Alphonce Meru amekiri kupokea shilingi Milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho na ameahidi kusimamia vyema fedha hizo huku Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi Eliurd Mwaitekele akisema atahakikisha kazi inamalizika ndani ya siku 90 kama ilivyopangwa.

Wakazi wa Koromije wakishiriki shughuli ya kusafisha eneo na kung’oa mawe kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Koromije.

Uondoaji miti kwa ajili ya upanuzi wa Kituo cha Afya Koromije

Wakazi wa Koromije wamefurahia upanuzi wa Kituo cha Afya Koromije.

Awali iliwalazimu kutembea hadi Sumve, Bukumbi, Sekou Toure ama Bugando kufuata huduma ya chumba cha kuhifadhi maiti hivyo serikali imesikia kilio chao na kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Mochwari.

Tazama BMG Online TV hapa chini 

SOMA Mkurugenzi Misungwi azungumza na Wanahabari

Recommended for you