Habari Picha

UTORO WA WANAFUNZI MASHULENI HUSABABISHWA NA KILIMO CHA TUMBAKU-AFISA ELIMU USHETU MKOANI SHINYANGA.

on

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na Shaban Njia
Sababu kubwa ya wanafunzi wa shule za sekondari katika Halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kuwa watoro mashuleni chanzo ni baadhi yao kuajiliwa na kutumikishwa shughuli ndogo ngogo kama kazi za vibarua kwenye Mashamba ya Tumbaku pamoja na kuajiliwa kazi za ndani.

Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Ushetu, Melkyada Gaka, aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na gazeti hili baada ya kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kilichofanyika katika Kata ya Nyamilangano kwa lengo la kujadili shughuli mbalimbali za maendeleo.

Gaka alisema kuwa kumekuwa na wimbi kubwa la utoro wa Wanafunzi hasa katika shule za Sekondari huku wengi wao wanakikimbilia Machimboni kwa ajili ya kusaka ajira ndogondogo na wengine kuajiliwa kazi za ndani wasichana na wavulana hali ambayo inafanya mahudhurio yao kuwahafifu mashuleni.

“Katika Halmashauri yetu ya Ushetu kweli kuna tatizo la Utoro mashuleni lakini mimi napendea kuzungumzia katika Wanafunzi wa Sekondari kwani hali mbaya kwani wanafunzi hawahudhurii mashuleni na wanaenda kutafuta ajira mijini za kufanya kazi za ndani na wengine katika mashamba ya Tumbaku”, Alisema Afisa Elimu huyo wa Sekondari katika Halmashauri ya Ushetu.

Aidha Afisa Elimu huyo aliendelea kusema kuwa sababu nyingine inayosababisha Utoro Mashuleni ni pamoja na umbali mrefu kutoka majumbani kwenda shuleni hali ambayo inasababisha Wanafunzi kukata tamaa pamoja na kutopenda masomo kutoka nauchovu wanaupata wa kutembea kila siku.

Hali hiyo ilikuja baada ya Diwani wa Kata ya saba Sabini Emanuel Makashi baada ya kufanya utafiti katika kata yake na  kubaini kuna utoro mwingi wa Wanafunzi uliokithiri hali ambauyo aliliomba Baraza Washirikiane na Halmashauri kuwahamasdisha Wazazi kuwapeleka watoto Mashuleni kuendelea masomo badala ya kuwakatishia njiani.

Makashi aliwataka wafanyakazi kutoka katika idara ya Elimu kuwaelimisha Wananchi juu ya suala la Elimu bure ikiwa ni pamoja na kuwanunulia Watoto wao sare za Shule kwani Wanafunzi wengine wamekuwa wakiogopo kwenda shule kwa ajili ya kuchekwa na wenzao ambao wenye sare za shule.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Idahina Yuda Lunyalula ambaye pia ni Mwenyekiti wa Serikali wa Kijiji cha Mwabomba alisema kuwa baadhi ya Wazazi wamekuwa wakiwaombea Watoto wao uhamisho wa kwenda kusoma shule nyingine na badala yake wanaenda kuwaozesha kwa lengo la kupata Mahali.

Hata hivyo alisema kuwa sababu nyingine inayochangia utoro mashuleni ni pamoja na Walimu kutoa adhabu nzito kwa Wanafunzi wanapokosea hali ambayo inawafanya Wanafunzi kushindwa kuendelea na masomo yao kutokana na hali hiyo na kuwataka Walimu kupunguza adhabu nzito kwa Wanafunzi.

Nae Mwenyekitio wa Halmashauri ya Ushetu Juma Kimisha alisema kuwa tatizo la utoro mashuleni linaonekana kuwa sugu na kuwataka Madiwani kuendelea kuripoti hali hiyo katika vyombo husika kwani Waratibu Elimu katika kata wanaonekana kuwa hawafanyi kazi  yao na kuwataka kuhakikisha kuwa wanafanya kazi yao ili kuhakikisha suala hilo linakwisha.

Recommended for you