Audio & Video

VIONGOZI WAFUNGUKA UZINDUZI WA KIPINDI KIPYA CHA UTPC

on

Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC umezindua kipindi kipya cha redio chenye maudhui ya kuhamasisha maendeleo katika jamii na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika jana Jijini Mwanza, Mkurugenzi wa UTPC, Abubakary Karsan alisema kipindi hicho kitakuwa kikirushwa kwenye redio 12 mkoani Mwanza na baadaye kitarushwa pia kwenye luninga mbalimbali nchini.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kipindi hicho, alitoa rai kwa wanahabari na vyombo vya habari kutumia fursa hiyo katika kuandaa vipindi vitakavyokuwa vikihamasisha maendeleo katika jamii.

Akizungumza kwa niaba ya wamiliki wa vyombo vya habari, Elirehema Kaaya ambaye pia ni Afisa Mahusiano halmashauri ya Jiji la Mwanza, alisema vyombo vyombo mbalimbali vya habari mkoani Mwanza vimeridhia kurusha kipindi hicho kwa ajili ya maendeleo ya jamii na kwamba maandalizi yake yatakidhi maudhui yenye ubora.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Mwanza, Osoro Nyawangah alitoa rai kwa viongozi mbalimbali wakiwemo wa serikali kutumia vyema kipindi hicho katika kushiriki mijadala mbalimbali ya kimaendeleo yenye kuutoa mkoa wa Mwanza kwenye orodha ya mikoa maskini nchini kwani ni mkoa wenye raslimali nyingi.

Tazama hapo juu Zitto Kamwe akihojiwa kwenye kipindi cha TUNAJADILIANA

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, akizungumza kwenye uzinduzi wa kipindi kipya cha TUJADILIANE kinachoandaliwa na UTPC

Mkurugenzi wa UTPC, Abubakary Karsan akizungumza kwenye halfa ya uzinduzi huo

Mwenyekiti wa MPC, Osoro Nyawangah akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi huo

Mwakilishi wa wamiliki wa vyombo vya habari, Elirehema Kaaya akizungumza kwenye halfa hiyo

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (kulia) akifafanua jambo wakati akihojiwa na mtangazaji Dotto Bulendu baada ya uzinduzi wa kipindi cha Tujadiliane ambapo mahojiano hayo yatarushwa kwenye kipindi hicho

Wanahabari mkoani Mwanza

Mgeni rasmi kwenye picha ya pamoja na watangazaji mbalimbali

Mgeni rasmi kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali

BMG Habari, Pamoja Daima

 

 

Recommended for you