Audio & Video

Shirika la Amref lakabidhi Ambulance mpya mkoani Simiyu

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Mkuu wa Mkoa Simiyu, Mhe.Antony Mtaka amelishukuru na kulipongeza shirika la Amref Health Africa kwa mchango wake mkubwa wa kuboresha huduma za afya katika mkoa huo.

Mhe.Mtaka alitoa pongezi hizo jana Mei 11, 2018 wakati akipokea gari la wagonjwa (Ambulance) lililotolewa na shirika la Amref kwa ajili ya hospitali teule ya mkoa wa Simiyu ambayo ilikuwa inakabiliwa na ukosefu wa gari hilo.

Mhe.Mtaka alisema shirika hilo kupitia mradi wake wa Uzazi Uzima limesaidia kuboresha huduma mbalimbali za afya mkoani Simiyu ikiwemo ujenzi na ukarabati Zahanati, Vituo vya Afya, wodi (Mama Ngojea) pamoja na kuwajengea uwezo wahudumu wa afya.

Meneja Programu ya Afya ya Mama na Mtoto, shirika la Amref nchini Tanzania Dr.Serafina Mkuwa alisema gari hilo lina thamani ya shilingi milioni 150 pamoja na kodi na kwamba limekabidhiwa kupitia mradi wa Uzazi Uzima unaolenga kupunguza vifo vya mama na mtoto kabla na baada ya kujifungua.

Shirika la Amref Health Africa linatekeleza miradi mbalimbai ya afya hapa nchini kupitia ufadhili ya serikali ya Canada.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Antony Mtaka akipokea Ambulance iliyotolewa na shirika la Amref Health Africa.

Meneja wa Programu ya Afya ya Mama na Mtoto kutoka shirika la Amref nchini Tanzania Dr. Serafina Mkuwa akizungumza wakati wa shughuli hiyo.

Meneja wa Programu ya Afya ya Mama na Mtoto kutoka shirika la Amref nchini Tanzania Dr. Serafina Mkuwa akizungumza wakati wa shughuli hiyo.

Mkurugenzi wa Shirika la Amref Canada, Onome Ako akitoa salami zake wakati wa makabidhiano ya Ambulance hiyo.

Katibu Tawala mkoani Simiyu, Jumanne Sagini akitoa salamu zake kwenye zoezi la makabidhiano ya Ambulance hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka akikata utepe kuashiria makabidhiano ya Ambulance hiyo. Wengine ni wawakilishi wa shirika la Amref Canada na Amref UK.

Makabidhiano ya Ambulance hii yamefanyika katika hospitali teule ya Mkoa wa Simiyu.

Ambulance hiyo ina thamani ya shilingi Milioni 150 pamoja na kodi.

RC Mtaka akionyesha ufunguo wa Ambulance hiyo.

Ambulance hiyo itasaidia kutoa huduma kwa wagonjwa wakiwemo wanaohitaji rufaa kwenda hospitali ya Kanda.

Baadhi ya wananchi na watumishi wa hospitali teule ya mkoa wa Simiyu wakishuhudia makabidhiano hayo.

Baadhi ya wananchi na watumishi wa hospitali teule ya mkoa wa Simiyu wakishuhudia makabidhiano hayo.

 

Tazama video hapa chini. 

Fungua BMG Habari kuhusu Mradi wa Uzazi Uzima.

Recommended for you