Audio & Video

Uzinduzi wa huduma katika bandari ya Mwanza Kusini hadi Portbell Uganda

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella amewahimiza wafanyabiashara ndani na nje ya nchi kutumia vyema fursa ya usafirishaji mizigo kupitia Ushoroba wa Kati (Central Corridor) unayohusisha njia ya reli na bandari.

Mhe.Mongella ameyasema hayo leo wakati akizindua usafirishaji wa mabehewa ya mizigo kwa kwa njia meli kupitia Ziwa Victoria kutoka bandari ya Mwanza Kusini (Tanzania) hadi bandari ya Portbell (Uganda), uliofanyika katika bandari ya Mwanza Kusini.

Uzinduzi huo umefanyika ikiwa ni miaka 10 imepita tangu huduma ya usafirishaji mizigo isitishwe katika bandari ya Mwanza Kusini (Tanzania) hadi bandari ya Portbell (Uganda) ambapo hatua hiyo italeta tija kwa wafanyabiashara wan chi zote mbili kwa kusafirisha mizigo kwa haraka na kwa gharama nafuu.

Hii ni ishara kwamba mizigo kutoka maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Dar es salaam itaweza kusafirishwa kwa njia ya reli hadi bandari ya Mwanza Kusini (Tanzania) na baadaye hadi bandari ya Portbell (Uganda) kupitia Ziwa Victoria ambapo meli ya MV.Umoja inayomilikiwa na Kampuni ya Huduma za Meli nchini (MSCL) itakuwa miongoni mwa meli zitakazosafirisha mizigo hiyo.

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa usafirishaji wa mabehewa ya mizigo kwa kwa njia meli kupitia Ziwa Victoria kutoka bandari ya Mwanza Kusini (Tanzania) hadi bandari ya Portbell (Uganda), iliyofanyika katika bandari ya Mwanza Kusini.

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella pamoja na viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria uzinduzi wa usafirishaji wa mabehewa ya mizigo kwa kwa njia meli kupitia Ziwa Victoria kutoka bandari ya Mwanza Kusini (Tanzania) hadi bandari ya Portbell (Uganda).

Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara TCCIA mkoani Mwanza, Elibariki Mmari akizungumza kwenye hafla hiyo

Mfanyabiashara Christopher Gachuma akizungumza kwa niaba ya wamiliki wa viwanda kwenye uzinduzi huo

Mabehewa yakiingizwa kwenye meli ya MV.Umoja inayomilikwa na Kampuni ya Huduma za Meli nchini MSCL

Mkuu wa Mkoa Mwanza na viongozi mbalimbali wakikagua eneo la mabehewa kuingilia kwenye Meli katika bandari ya Mwanza Kusini

Mizigo kutoka maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Dar es salaam itaweza kusafirishwa kwa njia ya reli hadi bandari ya Mwanza Kusini na baadaye bandari ya Portbell kupitia Ziwa Victoria

Wafanyabiashara mbalimbali Jijini Mwanza wakiwemo kutoka TCCIA

Wafanyabiashara mbalimbali wakifuatilia hafla hiyo

Tazama BMG Online TV hapa nchini

SOMA Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Uganda aipongeza serikali

Recommended for you