Audio & Video

Mwanza kuzindua kampeni ya “Furaha Yangu” wikendi hii

on

Na Judith Ferdinand, BMG

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kufanya vipimo vya Virusi vya Ukimwi, ikiwa ni uzinduzi wa kampeni ya Furaha Yangu ili kutambua afya zao.

Mhe.Mongella ametoa rai hiyo leo wakati akizungumza na wanahabari na kubainisha kwamba kampeni hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi mkoani Mwanza jumamosi Julai 21, 2018 katika uwanja wa Furahisha.

“Nawahimiza wakazi wa mkoa wa Mwanza hususani wanaume kuungana nami kwenye uzinduzi wa kampeni hii ili kujua hali ya afya mapema ambapo watakaobainika kuwa na maambukizi watapata fursa ya kuanza dawa mapema, kupata elimu ili kupunguza uwezekano wa kuwaambukiza wengine huku wakiishi kwa fuaraha”. Amehimiza Mhe.Mongella

Kwa upande wake Mganga Mkuu mkoani Mwanza Dkt.Thomas Rutachunzibwa amesema kiwango cha maambukuzi ya VVU kimepanda kutoka asilimia nne hadi hadi 7.2 hivyo kuna umuhimu wananchi wakashiriki kwenye kampeni hiyo hatua itakayosaidia kupambana na kiwango cha maambukizi ya virusi hivyo.

Recommended for you