Audio & Video

Kampuni ya Resolution Insurance yazindua huduma za bima Kanda ya Ziwa

on

Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi rasmi wa huduma za kampuni ya bima ya “Resolution Insurance” iliyofanyika jana jioni katika ukumbi wa Gold Crest Hotel Jijini Mwanza. Ofisi za kampuni hiyo ziko jengo la PPF Plaza ilipo Gold Crest Hotel ghorofa ya pili zikitazamana na chuo cha CBE.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Kampuni zinazotoa huduma za bima zimetakiwa kuwaelimisha wananchi ili wahamasike kujiunga na huduma hizo baada ya kutambua umuhimu wake.

Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella alitoa rai hiyo jana wakati akizindua rasmi huduma za bima za kampuni ya Resolution Insuration tawi la Mwanza, linalodhamiria kurahisisha huduma za bima kwa wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Mongella alisema bado watanzania wengi wakiwemo wanaojihusisha na shughuli za kilimo, ufugaji, uvuvi, wajasiriamali na wenye viwanda vidogo hawanufaiki na huduma za bima hivyo Resolution Insurance iweke mikakati ya kuwafikia wananchi hao.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Resolution Insurance, Maryanne Mugo alisema kampuni hiyo imedhamiria kuleta mabadiliko makubwa ya huduma bora za bima kwa wananchi wa Kanda ya Ziwa.

Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Kanda ya Ziwa, Sharif Hamad aliyahimiza makampuni ya bima kuhakikisha yanatoa huduma bora na kwa wakati ili kuwarahisishia wananchi upatikanaji wa huduma kiwemo afya.

Mkurugenzi Mkuu kampuni ya Resolution Inshurance, Maryanne Mugo akizungumzo kwenye hafla hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi kampuni ya Resolution Insurance, Zuhura Muro akizungumza kwenye hafla hiyo.

Meneja wa Resolution Insurance tawi la Mwanza, Curtis Mukami akizungumza kwenye hafla hiyo.

Meneja Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Kanda ya Ziwa, Sharif Hamad akizungumza kwenye hafla hiyo.

Mgeni rasmi, wajumbe wa bodi pamoja na menejimenti ya Resolution Insurance wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Mkuu wa Mkoa Mwanza akiwa pamoja na wajumbe wa bodi ya Resolution Insurance.

Mkuu wa Mkoa Mwanza akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Resolution Insurance.

Mkuu wa Mkoa Mwanza akiwa kwenye picha ya pamoja na Menejimenti ya Resolution Insurance.

Baadhi ya wafanyakazi wa Resolution Insurance. 

Wafanyakazi wa Resolution Insurance.

Mdau wa Resolution Insurance kutoka BKM Insurance akiwa kwenye hafla hiyo.

Mshereheshaji MC.Charz Machugu kutoka Sahara Media.

Mwimbaji Zarry Edosha akitumbuiza kwenye hafla hiyo. 

SOMA Mapokezi ya Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda Jijini Mwanza

Recommended for you