Habari Picha

UZINDUZI WA BOMBA LA MAFUTA MKOANI TANGA

on

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli leo Agost 03,2017 amewasili mkoani Tanga kwa ajili ya ziara ya kikazi mkoani humo.

Pamoja na shughuli nyingine, shughuli kubwa inayotarajiwa kufanywa na Rais Magufuli ni pamoja na ile atakayoungana na Rais wa nchi jirani ya Uganda Mhe.Yoweri Kaguta Museveni kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga hapa nchini.

Zoezi hilo linatarajiwa kufanyika kesho kutwa Agost 05,2017 Chongoleani mkoani Tanga ambapo macho na maskio ya watu wote katika nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu yataelekezwa huko ikizingatiwa kwamba hii ni fursa ya kipekee kwa Tanzania kwani mradi huo ulikuwa ukiwania na nchi nyingine zaidi ya Tanzania kutokana na umuhimu wake kiuchumi. Rais Museveni anatarajiwa kupokelewa kesho na mwenyeji wake, Rais Magufuli.

Ujenzi wa bomba hilo unatarajiwa kugharimu shilingi Trilioni Nane hadi kukamilika kwake kmwaka 2020 ambapo hadi kukamilika kwake utakuwa umetoa ajira za moja kwa moja zipatazo 10,000 na ajira zaidi ya 30,000 zisizo za moja kwa moja zitokanazo na wananchi kujiajiri ikiwemo kuuza vyakula ikizingatiwa kwamba bomba hilo pia litapita katika mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Dodoma na Manyara.

 

Recommended for you