Audio & Video

UZINDUZI WA FILAMU YA MAGWANGALA WAINGIA DOSARI MKOANI GEITA

on

BMGHabari

Jana Julai 27,2017 uzinduzi wa filamu mpya ya Magwangala iliyoandaliwa na waigizaji wa mkoa wa Geita uliingia dosari baada ya kutofanyika huku wakazi wa Mji wa Geita na maeneo jirani waliojitokeza kushuhudia uzinduzi huo wakiondoka eneo la tukio kwa gadhabu.

Kwa mjibu wa Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji mkoani Geita, Rose Michael a.k.a Rose Bonanza, uzinduzi huo ulipaswa kufanyika katika ukumbi wa Desire Park Resort kuanzia majira ya saa moja jioni ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Anastazia Wambura.

Lakini hadi majira ya saa sita usiku, hakuna kilichokuwa kikieleweka hali iliyowalazimu watu kuondoka eneo la uzinduzi huku duru za habari zikizagaa kwamba kwamba uzinduzi huo uliingia dosari kutokana na malalamiko ya mgodi wa GGM kudai kwamba filamu hiyo imejaa uchochezi.

Eneo la tukio wahusika hawakuwepo na hata mgeni rasmi hakufika huku ikielezwa kwamba kulikuwa na kikao katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita usiku huo, kuhusiana na uzinduzi wa filamu hiyo tayari iliisha kaguliwa na Bodi ya Filamu Tanzania na kupewa kibali cha kuwafikia watazamaji.

Tunafuatilia zaidi undani wa kilichotokea na tutawajuza wapenzi wetu wa BMG.

TUJIKUMBUSHE

Soma zaidi HAPA kuhusu uzinduzi huo

 

Recommended for you