Habari Picha

KLABU YA BIASHARA YA BENKI YA NBC YAZINDULIWA JIJINI MWANZA

on

George Binagi @BMG

Benki ya NBC imefanya imezinduzi wa Klabu ya Biashara ya NBC ijulikanao kama “NBC Business Club” Jijini Mwanza, lengo likiwa ni kuwaweka pamoja kwa ajili ya manufaa mbalimbali ikiwemo mafunzo.

Mafunzo yanayotolewa kwenye klabu hiyo yamelenga kukuza na kuendeleza biashara za wafanyabiashara waliojiunga ambapo yanatolewa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC, Mamlaka ya Mapato nchini TRA pamoja na Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo, amesema hatua hiyo itasaidia kuwaweka pamoja wafanyabiashara wa mkoa wa Mwanza na kuipongeza benki ya NBC kwa mkakati huo.

Aidha amekaribisha ushirikiano wa benki ya NBC pamoja na wafanyabiashara wote mkoani Mwanza katika kufanikisha adhima ya serikali juu ya ujenzi wa viwanda na kuwahakikishia miundombinu bora katika kutimiza adhima hiyo.

Kaimu Mkurugenzi wa benki ya NBC nchini, Theobald Sabi amesema klabu ya biashara ya NBC (NBC Business Cluba), inatoa huduma zisizo za kifedha kwa wafanyabiashara kupitia mafunzo maalumu ya ujuzi wa biashara na kuwajengea uwezo wa kuendesha biashara zao ndani na nchi ya nchi.

Kaimu Mkurugenzi wa benki ya NBC nchini, Theobald Sabi, akizungumza kwenye uzinduzi huo, ambapo amewasihi wafanya bishara kujiunga na klabu hiyo ili kunufaika na fursa zilizopo. Kushoto ni Filbert Mponzi ambaye ni Mkurugenzi huduma kwa wateja binafsi/ rejareja benki ya NBC

Mkurugenzi wa bodi ya benki ya NBC, Dr.Kassim Hussein akizungumza kwenye uzinduzi huo

Meneja Mahusiano benki ya NBC, William Kallaghe akizungumza kwenye uzifunzi huo

Baadhi ya washiriki wa NBC Business Club mkoani Mwanza

Baadhi ya washiriki wa NBC Business Club mkoani Mwanza

Washiriki

Picha ya pamoja kati ya washiriki wa NBC Business Club, viongozi mbalimbali wa benki ya NBC pamoja na mgeni rasmi.

Recommended for you