Makala

Hili ni chukizo kwa Mungu na ni kinyume na maana halisi ya Siku ya Wapendanao

on

Jina “Valentino” ni jina la Mtakatifu wa Kiroma aliyeitwa Valentino. Siku ya Mtakatifu Valentino hufahamika kama Siku ya Wapendanao “Valentine Day”, ikiwa ni maadhimisho ya kila mwaka, yaani kila tarehe 14 Februari, watu husherehekea upendo na kuthaminiana na kujaliana kati ya watu wenye uhusiano binafsi na mara nyingi hutumika kwa mahusiano ya kimapenzi.

Siku hii asili yake ni baada ya wakristo wa zamani kuteswa hadi kufa kwa ajili ya kuupenda Ukristo. Kihistoria Mtakatifu Valentino alitumika kama kiongozi wa dini kanisani katika utawala wa Mfalme Claudia.

Mfalme Claudia alimkamata Mtakatifu Valentino na kumfunga. Mtakatifu Valentino aliteswa kwa ajili ya Imani yake ya Ukristo na kufa tarehe 14 mwezi Februari, 269 AD. Kwa ajili ya msimamo na Imani yake na kufa kwa kutetea Ukristo, Papa Gelasius aliitangaza tarehe 14 mwezi Februari mwaka 496 AD kuwa siku ya Mtakatifu Valentino.

Jinsi watu wanavyo ichukulia siku hii ni kutokana na tabia zao zilivyo au kiasi cha hofu ya kumuogopa Mungu kilivyo. Watu wengi huichukulia siku hii kama ni siku ya mapenzi, wengine hufanya kama siku ya kujenga mahusiano upya, kupatana na wapendwa wao au kufurahi na wale wanaowapenda.

Mbaya zaidi baadhi ya watu huchukulia siku hii kama ni siku ya kufanya maovu na ufuska. Hili ni chukizo kwa Mungu na ni kinyume na maana halisi ya Siku ya Mtakatifu Valentino (Valentine Day). Ni bora tuichukulie siku hii kidini zaidi kama waasisi wa Valentine walivyofanya.

Mungu aliupenda ulimwengu na kumtoa mwanawe kama kafara ya dhambi zetu. Ni vizuri tukitumia mda tulio nao kujitakasa na kutubu dhambi zetu. Je sisi ni nini mbele za Mungu zaidi ya wale waliokuwa wanachinjwa na kuuawa kikatili kwa ajili ya kulinda imani yao? HADI PUMZI YAO YA MWISHO WALIMTAMKA KRISTO. Tuwaenzi kwa kutenda wema tu.

Kile kidogo ulichonacho, jaribu kukitumia na ndugu, jirani, rafiki, watu wasiojiweza na watoto wanaoishi mtaani. Naamini utabarikiwa zaidi. Hiyo ndiyo maana halisi ya Siku ya Wapendanao.

Kwa Msaada wa Mtandao

Recommended for you