Audio & Video

VIWANDA: Vijana na wanawake kupewa bure maeneo kuwekeza

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji Dkt. Charles Mwijage amewataka wakurugenzi wote wa Halmashauri nchini kutekeleza kwa vitendo agizo la Makamu wa Rais Mama Samia Hassan la kutenga maeneo kwa ajili ya akina mama na vijana wanaowekeza katika sekta ya viwanda.

Dkt. Mwijage alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika katika viunga vya Rock City Mall ambayo yanaandaliwa na chemba ya wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo TCCIA.

Alisema halmashauri nchini zinapotenga viwanja na majengo kwa ajili ya wafanyabiashara na wawekezaji, lazima itenge maeneo ya bure kwa ajili ya akina mama na vijana wanaoanza uwekezaji kwani wengi wao hawana mitaji wala dhamana za kukopesheka hivyo lazima serikali iwazeshe kupitia azma yake ya serikali ya viwanda.

Mwenyekiti wa TCCIA mkoani Mwanza, Dkt. Elibariki Mmari ameiomba serikali kutenga eneo maalum kwa ajili ya maonesho hayo na kwamba taasisi hiyo iko tayari kuboresha eneo hilo.

Alisema lengo la maonesho hayo ni kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa Afrika Mashariki kutangaza bidhaa zao, kujenga mahusiano na kuunga mkono soko la Afrika Mashariki hivyo aliomba serikali kuhakikisha inasaidia kuondoa vikwazo na kuboresha mazingira ya kufanya katika meneo ya mipakani.

Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya maendeleo ya biashara nchini TANTRADE, Edwin Rutageruka alisema taasisi hiyo iko tayari kuboresha viwanja vya Nyamhongolo maaruku kama Nane Nane ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara kuonyesha bidhaa zao katika eneo linalokidhi vigezo.

Aidha alisema jukumu kubwa la TANTRADE ni kuwaunganisha wazalishaji wa bidhaa mbalimbali na masoko ndani na nje ya nchi hivyo wakurugenzi wa halmashauri watumie fursa hiyo kueleza bidhaa zinazozalishwa kwenye halmashauri zao na taasisi hiyo itazitafutia masoko.

Waziri Mwijage akikagua mabanda mbalimbali
Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji Dkt. Charles Mwijage akizungumza kwenye ufunguzi wa maonesho ya biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza
Mwenyekiti wa TCCIA mkoani Mwanza, Dkt. Elibariki Mmari akizungumza kwenye ufunguzi huo
Mkurugenzi wa Mamlaka ya maendeleo ya biashara nchini TANTRADE, Edwin Rutageruka akieleza mchango wa taasisi hiyo katika kukuza soko la bidhaa mbalimbali nchini
Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji Dkt. Charles Mwijage, akijiandaa kukata utepe kama ishara ya ufunguzi wa maonesho ya biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza
Banda la jeshi la polisi
Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji Dkt. Charles Mwijage alipotembelea banda la jeshi la polisi
Washiriki waliojiandaa vyema kushiriki maonesho hayo walipewa zawadi za vikombe na vyeti vya utambuzi
Tazama BMG Online Tv hapa chini

Recommended for you